Kundi la Original Comedy Matatani Kwa Kuvaa Sare za Jeshi la Polisi Kwenye Sherehe ya Masanja Mkandamizaji



katika siku za hivi karibuni, kumejitokeza tabia kwa baadhi ya watu wakiwemo wasanii watu wengine mmoja mmoja kutumia mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na usalama hapa nchini likiwemo
Jeshi la Polisi katika shughuli zao za kisanii au katika kazi mbalimbali, Jambo ambalo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za Nchi.

Kwa mujibu wa Sheria ya kanuni za makosa ya Jinai, sura ya 16 na marejeo yake ya mwaka 2002, kifungu cha 178 (1) na (2) kinachozungumzia makosa dhidi ya sare za majeshi ya ulinzi na usalama, kinabainisha wazi kuwa ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama kuvaa mavazi yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi hayo bila kibali kutoka kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kufuatia kitendo kilichofanywa na kundi la kisanii la “ Original Comedy” kuvaa mavazi yanayoshabihiana na sare za Jeshi la Polisi, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam linachukua hatua za kisheria dhidi ya wasanii hao.

Aidha Jeshi la Polisi nchini, linatoa onyo kali kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa na majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini na atakayebainika hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi yake.(Video:Masanja Mkandamizaji akitoa adhabu kwa MC Pilipili kwa kuchelewa kuoa
Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wale wote wenye mavazi yanayoshabihiana na sare za majeshi ya ulinzi na usalama kuzisalimisha mara moja katika vituo vya Polisi vilivyokaribu nao.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba – Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Makao Makuu ya Polisi. 
 Habari za Magazetiya Leo Jumanne August 16, 2016 bofya hapa

MANJI AJIUZULU YANGA bofya hapa







Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top