Kamishna Wa TRA Azindua Kampeni Ya Uhakiki Wa Namba Ya Mlipa Kodi (TIN)

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imewataka wafanyabiashara katika jiji la Dar es salaam kuboresha taarifa za usajili wa namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) ili kuondokana na mfumo wa kizamani wa usajili wa namba hiyo.


Uhakiki huo utaiwezesha mamlaka hiyo kuweza kujua idadi sahihi ya wafanyabiashara walipa kodi, kuondoa walipa kodi hewa ambao wamekuwa hawajihusishi na biashara kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo au kufungwa kwa makampuni yao.


Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ndugu Alphayo Kidata alisema mfumo huo utawawezesha wafanyabiashara kulipa kodi kwa gharama nafuu sambamba na kuweka mazingira ya ulipaji kodi kwa hiari.


Kidata alisema kuwa mfumo wa sasa wa uhifadhi kumbukumbu za walipa kodi ulikuwa na kasoro nyingi hivyo mfumo mpya utaendana na ukuaji wa teknolojia na kukuza uchumi.


“Zoezi hili linamtaka kila mwenye namba ya utambulisho yani TIN kufika katika ofisi za TRA zilizopo karibu naye bila kuwakilishwa na mtu yeyote na zoezi litatumia dakika 10 kumalizika” alisema


Naye Elija Mwandubya ambaye ni kamisha wa mapato wa ndani wa mamlaka hiyo, alisema zoezi hilo litachukua siku 60 na kuanzia Dar es salaam na baadaye kuhamia mikoa mingine ndani ya nchi.


“TRA ina wafanyabiashara walipa kodi milioni mbili na laki moja hivyo uboreshwaji wa TIN utatupa uelewa wa idadi kamili ya walipa kodi”Alisema


Elija alisema kutakuwa na vituo maalum kwaajili ya uhakiki wa taarifa katika mikoa ya kikodi ambapo Kinondoni wafanyabiashara watatakiwa kutembelea ofisi za TRA zilizopo jengo la LAPF – Kijitonyama na Kibo Complex Tegeta.


Ilala wafanyabiashara watembelee ofisi ya TRA shauri moyo na 14 Rays Gerezani na Temeke wafike ofisi za uwanja wa Taifa.
Habari zzilizopo katika Magazeti ya Leo Jumatano August 17, 2016 bofya hapa

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top