Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania asimamishwa kazi kwa uzembe

Waziri wa Ujenzi Prof. Makame Mbarawa amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege ATCL Kapten Johnson Mfinanga na Mkurugenzi wa Uendeshaji Kapten Sadick Muze kwa kosa la kumchagua rubani asiye na sifa kwenda kupata mafunzo Canada.

Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Mbarawa amesema marubani watano walichaguliwa kwenda nchini Canada kwa ajili ya kupata mafunzo ya kurusha ndege mpya zitakazoingia nchini mwezi Septemba kama alivyoahidi Rais Dkt. John Magufuli.


Waziri ameongeza kuwa baada ya kukamilika kwa malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mbili mpya za shirika la ATCL alitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi huyo kuchagua marubani watano wenye sifa kwa ajili ya kwenda kupata mafunzo nchini Canada ambapo kati ya watano waliochaguliwa mmoja amebainika hana vigezo hivyo ameamua kuwasimamisha viongozi hao kutokana na uzembe.


Aidha waziri Mbarawa amewataka watendaji wa serikali kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na kanuni za kazi na mtumishi atakayefanya kinyume hatasalimika kuwajibishwa.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top