
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro
Mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni jambazi, ameuawa eneo la Mabibo Loyola baada ya kukutana na kikundi cha ulinzi shirikishi jana saa tisa usiku na kuzua tafrani.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na wenzake wanne huku kila mmoja akiwa amebeba begi mgongoni.
Alisema baada ya kikundi hicho kuwaona waliwatilia shaka watu hao na kuwasimamisha kwa lengo la kuwahoji lakini walikimbia na kumkamata mmoja. “Baada ya kukamatwa alianza kuwatishia kuwa atawaua ghafla aliingiza mkono mfukoni na kutoa kitambaa na kukitupa chini kisha akalipua bomu,” alisema Kamanda Sirro.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)