IJUE SHERIA ILIYOIPELEKA MO BEJAIA NUSU FAINALI CONFEDERATION CUP


Na Patrick Sungura.

Kumekuwa na mijadala mingi baada ya Mouloudia Olympique de Béjaïa (MO BEJAIA) kufuzu hatua ya nusu fainali ya CAF CONFEDERATION CUP 2016 licha ya kuwa sawa points na timu ya Medeama ya Ghana, zote kwa pamoja zikipata points 8 katika hitimisho ya hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.

Timu hiyo inayotoka mjiwa Bejaia, nchini Algeria na inayotumia uwanja wa Stade de l’Unité Maghrébine imefunzu hatua ya nusu fainali kwa mujibu washeria zinazoongoza mashindano hayo, sheria hiyo inayopatikana kwenye andiko linalosomeka “CAF CONFEDERATION CUP REGULATIONS”, sura ya tatu inayosomeka “FIXTURES AND FORMAT OF THE COMPETITION” na kifungu cha 20 na kifungu kidogo cha kwanza, kama zinavyoonekana hapo chini;



KwaTafsiriisiyorasmiyakifungu cha 20.1 ni “Idadikubwaya point/alamazilitopatikana katikamechi zilizokutanisha timu husika”

Medeama na Mo Bejaia zilikutana mara mbili katika hatua ya makundi, Mechiya kwanza iliyochezwa Sekondi-Takoradi Stadium, Sekondi-Takoradi tarehe 29/06/2016, ilimalizika kwa sare ya bilakufungana na kuziweshezatimu hizo husika kupata pointi moja na mechi ya pili iliyochezwa Stade de l’Unité Maghrébine, Béjaïa, tarehe 23/08/2016 nakumalizika kwa MO Bejaia kupata ushindi wa goli moja kwa sifuri na kuiwesheza timu hiyo kupata points 3 muhimu, hivyo katika mechi hizi mbili MO Bejaia imeweza kupata alama nyingi ambazo ni alama 4 na kuwazidi wapinzani wao Medeama iliyokusanya alama mojatu.

Kama sheria inayoeleza MO Bejaia inapata nafasi ya kuungana na TP Mazembe kupata nafasi ya kuendelea hatua ya nusu fainali ikiwaacha Medeama naYanga zote kutoka kundi lao la A.

Baada yakufuzu hatua ya Makundi TP Mazembe na MO Bejaia zitamenyana na washindi wa Kundi B ambaoni FUS Rabat ya Morocco na Étoile du Sahel ya Tunisia.

Mechiza kwanza za hatuaya Nusu fainali zinatarajiwa kuwa tarehe 16 hadi 18 ya mwezi September ambapo TP Mazembe itakutana na Étoile du Sahel na FUS Rabat itapambana na MO BEJAIA.
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top