CRISTIANO RONALDO MCHEZAJI BORA WA ULAYA


 
Cristiano Ronaldo amewashinda wwachezaji Antoine Griezman na Gareth Bale na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya kwa upande wa wanaume. Ushindi huu umetokana na mafanikio yake msimu uliokwisha huku akiwa ametwaa vikombe vikubwa vya ulaya kwa maana
klabu bingwa ulaya na kombe la mataifa ya Ulaya.

Ronaldo pia alikuwa mfungaji bora wa Ulaya huku akiwa wa pili kwa ufungaji katika ligi kuu ya nchini Hispania. Ikumbukwe pia, Ronaldo alifika fainali hizi huku mpinzani wake akiwa ni Antoine Griezman na kumshinda kote ijapokuwa kwenye fainali ambayo Ureno walitwaa ubingwa aliumia mapema sana.

Ronaldo alifunga mabao 51 kwenye mechi 48 msimu uliopita huku akifunga mabao 3 pekee kwenye mashindano ya mataifa ya Ulaya ambapo mchezaji Antoine Griezman alikuwa mfungaji bora.



Yaome maswali na majibu aliyoyajibu Ronaldo baada ya kutwaa tuzo hiyo huku pia akiwapongeza wachezaji wenzake waliofika kwenye hatua ya mwisho ya kinyang’anyiro hiki, Bale na Griezman.


Katika hatua nyingine mchezaji Ada Hegerberg ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa ulaya kwa upande wa akina dada





CHADEMA Wamwalika Kamanda Sirro Katika Maandamano yao ya UKUTA Bofya hapa

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top