Wazungu wamwalika mtengeneza helkopta wa Tunduma Ndugu Adam Kinyekile



Wananchi wakitazama helikopta iliyotengenezwa na Adam Kinyekile. 

 Mkazi wa Tunduma mkoani Songwe, Adam Kinyekile (34) ambaye ametengeneza helikopta amepata mwaliko maalumu wa Wazungu kutoka Afrika Kusini, ili kutembelea kiwanda chao cha kutengeneza
chopa.

Kinyekile ambaye pia ni fundi magari, alitumia ubunifu wake kuunda helikopta iliyomvutia Kiongozi wa Mbio za Mwenge, George Mbijima akiwa mjini Tunduma ambaye alimtembelea kisha kuweka jiwe la msingi kwenye helikopta hiyo.


Hata hivyo, baada ya taarifa za kijana huyo kurushwa kwenye vyombo vya habari, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ilipiga marufuku mtu yeyote kujihusisha na utengenezaji, au ubunifu wa ndege bila kufuata taratibu.


Onyo hilo lilionekana kumlenga Kinyekile kwa kazi yake, jambo ambalo lilisababisha asiendelea na maboresho ya helikopta yake licha ya kudai ilikuwa imebaki kurushwa.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top