VIDEO: Tazama jinsi Chui alivyomvamia mwanamke katika hifadhi, China

Mtu mmoja amepoteza maisha na mwingine mmoja kujeruhwa baada ya kuvamiwa na Chui walipokuwa katika moja ya hifadhi ya wanyama iliyopo Beijing, China.Tukio hilo lilitokea baada ya mmoja wa watembeleaji wa eneo hilo kutoka katika gari alilokuwa amepanda na kwenda upande wa pili wa mtu ambaye walikuwa naye pamoja katika gari hilo na ndipo chui alipomvamia na kumvuta.

Katika video ambayo ilichukuliwa na kamera ambayo ipo hifadhini hapo inaonyesha kuwa baada ya chui kumvuta na wenzake wawili kumfuata na ili kumsaidia lakini ilishindikana na chui huyo kumjeruhi mwingine.

Baada ya kutokea tukio hilo, taarifa kutoka China zinazeleza kuwa kwa sasa hifadhi hiyo imefungiwa kwa muda ili kupisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Aidha inaelezwa kuwa hifadhi hiyo imekuwa ikiwaruhusu watu ambao wanaokwenda kuangalia wanyama kutumia magari yao wenyewe kama watapenda kufanya hivyo.


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top