UN yajadili mapigano Sudan Kusini


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya kikao cha dharura kuzungumzia mapigano yaliyoanza tena nchini Sudan Kusini.

Mamia ya Watu wameuawa tangu kuzuka kwa mapigano hayo Alhamisi iliyopita hadi sasa, katika mji mkuu
wa nchi hiyo Juba.

Mapigano hayo ni kati ya vikosi vinavyomuunga mkono Rais wa nchi hiyo Salva Kiir na yale yanayoongozwa na Makamu wa Rais Riek Machar.

Viongozi hao wawili hivi karibuni walisaini makubaliano ya amani ya kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa miaka miwili.

Awali Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezielezea ghasia hizo zilizoanza tena Sudan kusini, kama zisizo na sababu na hazikubaliki. Amewataka viongozi hao kuyaagiza majeshi yao kujiondoa katika mapigano.

Kwa upande wake Mjumbe wa Umoja wa Mataifa, Sudan kusini Shantal Persaud amesema kambi za pande zote mbili mjini Juba zimeshambuliwa na silaha nzito. Hali inayotishia mamia ya raia kujikuta kuwa wakimbizi.

Aidha amewekea matumaini ya kutekelezwa kwa Makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwaka uliopita.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top