Watu walikuwa wamekusanyika kusherehekea Sikukuu ya Bastille
Zaidi ya watu 80 wameripotiwa kuuawa katika shambulio lililotokea katika mji wa Nice kusini mwa Ufaransa
.Lori lililokuwa likienda mwendo kasi lilijiingiza katika mkusanyiko wa watu waliokuwa wakiangalia maonesho ya fataki kuadhimisha siku ya kitaifa ya Bastille, ambayo huja na shamra shamra kila mwaka.
.Lori lililokuwa likienda mwendo kasi lilijiingiza katika mkusanyiko wa watu waliokuwa wakiangalia maonesho ya fataki kuadhimisha siku ya kitaifa ya Bastille, ambayo huja na shamra shamra kila mwaka.
Mwendesha mashtaka katika mji wa Nice, Jean- Michel Pretre amesema lori hilo liliendelea kutembea kilo mita mbili kabla ya polisi kumpiga risasi dereva.
Bunduki na makombora yameripotiwa kukutwa ndani ya lori hilo.
Waakazi wa mji huo wa Nice wameshauriwa kutulia majumbani.Lori lililotumiwa na mshambuliaji
Rais Francois Hollande amerudi mjini Paris kwa ajili ya kufanya kikao cha dharura.
Hali ya tahadhari iliyowekwa toka kutokea kwa shambulio lililofanywa na Islamic State mjini Paris, bado iko palepale nchini Ufaransa.
Nafasi za Kazi, Maombi yatumwe kabla ya Agust 15, 2016 Bofya hapa
Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Ijumaa July 15, 2016 Bofya hapa
Nafasi za Kazi, mwisho wa kutuma maombi July 27, 2016 Bofya hapa
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)