Samir Nasri amepigwa marufuku hadi apunguze uzani wake
Kiungo cha kati wa Manchester City Samir Nasri amepigwa marufuku kushiriki mazoezi ya pamoja baada ya kuongeza uzani kupindukia
Kocha Pep Guardiola amethibitisha kuwa sababu yake kumuacha nje kiungo huyo ni kunenepa.
Nasri, 29, aliachwa nje hata baada ya wachezaji wote wa akiba kutumika katika mechi dhidi ya Borussia Dortmund nchini China.
Hapo jana mlinzi Gael Clichy alitambua sababu ya kukosekana kwa baadhi ya wachezaji katika kambi ya mazoezi kuwa ni kunenepa.
Meneja huyo mpya wa Manchester City Pep Guardiola amewapiga marufuku wachezaji waliozidi uzito, kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza.
Pep amesema uzito ni jambo muhimu na kuwa wachezaji lazima waepuke baadhi ya vyakula na vinywaji.
Shoka la Guardiola lamuangukia Nasri
Kumhusu Nasri, Guardiola amesema kuwa alirejea Uingereza baada ya likizo akiwa amenenepa.
Mfaransa huyo sasa atalazimika kufanya kila awezalo kurejea katika kikosi cha kwanza baada ya kukosa takriban nusu ya msimu uliopita baada ya kupata jeraha la paja.
''Alijeruhiwa msimu uliopita kwanini ?
tungependa wachezaji wetu kuwa wenye siha nzuri na unene wastani ili wanapoingia uwanjani wanakimbia hata kwa dakika 90 kama Fernandinho na [Aleksandar] Kolarov.
Natarajia katika majuma mawili yanayofuata tutakuwa katika hali nzuri kiafya.

Haya hapa majina 1,091 ya wadaiwa yaliyotangazwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu bofya hapa
Habari zilizopo katika Magazeti ya leo alhamisi July 28, 2016 bofya hapa
Breaking News: IRINGA: Askari aliyemuua mwanahabari Daudi Mwangosi ahukumiwa kufungwa Jela bofya hapa
Breaking News: IRINGA: Askari aliyemuua mwanahabari Daudi Mwangosi ahukumiwa kufungwa Jela bofya hapa
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)