SABABU YA WACHEZAJI WENGI WEUSI KWENYE KIKOSI CHA UFARANSA


Moja kati ya ‘ishu’ ambayo ime-trend sana kwenye social media si za kibongo pekee bali hata za mataifa ya Ulaya pamoja na vyombo vyao vingine vya habari ambavyo navyo vimeripoti kwa ukubwa, ni uwepo wa wachezaji wengi weusi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa ambacho kimeonekana kikiwa na wachezaji wengi wenye asili ya Afrika.

Nimeona kuna haja ya kulizungumzia hili ili kuweza kuona sababu ya timu ya Ufaransa kuwa na wachezaji wengi wenye asili ya Afrika.

Historia ya Ufaransa na nchi za kiafrika

Ufaransa ilitawala baadhi ya nchi za kiafrika hususan za ukanda wa Afrika ya Magharibi na baadhi ya nchi za ukanda wa Kaskazini ndiyo maana unaona kuna wachezaji wengi kutoka kwenye nchi za kiafrika kutoka ukanda huo, mfano nchi kama Senegal, Guinea, Algeria, Morocco n.k. Asilimia kubwa ya wachezaji wa Ufaransa wenye asili ya Afrika wanatoka kwenye nchi ambazo zilikuwa makoloni ya taifa hilo.

Lakini kama mfuatiliaji mzuri wa historia, sio kizazi hiki cha akina Zidane, Viera, Makelele, wachezaji wengi ambao wana asili ya Afrika waliocheza timu ya taifa ya Ufaransa. Lakini tangu zamani historia inatuambia kwamba, wakazi wengi wa Ufaransa ni wahamiaji. Ukirudi nyuma miaka ya 1960 wachezaji ambao walikuwa wanacheza timu ya taifa kwa wakati huo walikuwa ni wahamiaji wa watu kutoka Austria, Czech Slovakia, Italy na mataifa mengine.

Ukirudi miaka 30 nyuma unakutana na Michel Platini, Platini ni mototo wa wahamiaji kutoka Italy, kwahiyo Ufaransa kwa asilimia kubwa ya watu wa hapa ni wahamiaji.

Tukirudi kwenye miaka ya hivi karibuni, baada ya Ufaransa kuchukua ubingwa wa dunia wa mwaka 1998 kulikuwa na kitu kiliitwa ‘blanc-black-blue’ wakimaanisha, blanc-watu weupe (wazungu), black-watu weusi, (wenye asili ya afrika) na blue-waarabu. Hii ilileta maneno mengi sana kwasababu hakukuwa na alama ya timu ya taifa ya Ufaransa licha ya kuchukua ubingwa lakini ukiiangalia timu haileti taswira ya Ufaransa.

Inaonekana wachezaji wengi wanatoka kwenye mataifa mbalimbali hususan Afrika, kwahiyo wakawa wanatafuta jinsi ya kupunguza jambo hilo ili siku za mbele wawepo wachezaji wazawa wanaocheza kwenye kikosi cha Ufaransa wawe ni wazawa.

Kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 2010 Afrika Kusini kuna tukio la mgomo lilitokea baada ya baadhi ya wachezaji kususia mazoezi wakiongozwa na Patrice Evra, Nicolas Anelka, Frank Ribery. Ufaransa haikufanya vizuri kwenye michuano ya mwaka huo.

Ufaransa inaweka mpango mkakati wa kupunguza wachezaji ambao si wazawa kwenye timu ya taifa

Baada ya hizo vurugu zilizotokea, na matokeo mabovu Ufaransa waliyoyapata kwenye fainali hizo wakaja na mpango mkakati wa kupunguza idadi ya wachezaji ambao siyo wazawa na kutengeneza mpango wa kutengeneza idadi ya vijana wazawa ili siku za usoni wawe wengi na kuwakilisha timu ya taifa ya Ufaransa.

Kupunguza vijana wasio wazawa kutoka asilimia 70 katika vituo vya kukuzia vipaji ambako asilimia kubwa ya vijana ilikuwa ni wachezaji wenye asili ya kiafrika na kiarabu, kwahiyo wakaamua kupunguza kutoka asilimia 70 na badala yake wawe wanasajili wageni kwa asilimia 30 tu asilimia 70 ibaki kwa wazawa, zoezi ambalo lilifanyika.

Mpango wa kupunguza wachezaji wasio wazawa wa Ufaransa unafeli

Ilipofika mwaka 2012/13 walewale makocha wa timu za taifa za vijana za Ufaransa chini ya umri wa miaka 16, 17, 18, 19, 20, 21 wakawa wanahitaji wachezaji wenye nguvu. Moja kwa moja wachezaji wenye nguvu ni wale vijana wenye asili ya kiafrika akina Paul Pogba, Kareem Benzema, na wachezaji wengine ambao unawaona wanacheza kwasababu walihitajika kutokana na wana nguvu.

Kwahiyo ule mfumo wa kutaka kuibadilisha timu ya Ufaransa kuwa ya wazawa zaidi ukafa wenyewe ikabidi kuwapa nafasi vijana wenye asili ya kiafrika kwasababu tayari mahitaji yalikuwa ni vijana wenye nguvu na vijana wenye nguvu ni waafrika.

Lakini jambo jingine, kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa michezo, kuna mchezo wa rugby ambao ni maarufu sana Ufaransa, shuleni wamegawanyika, wazungu wao wanapenda sana watoto wao wacheze mchezo wa rugby ndiyo maana leo hii wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa ya rugby inaundwa na wachezaji wote wazungu.

Kuanzia chini kwenye ngazi za shule, watoto wadogo wenye asili ya Afrika na asili ya kiarabu wanachipukia kwenda kucheza soka wakati watoto wa kizungu ambao ndio wenye asili ya kifaransa wao wanakwenda kucheza rugby. Kwahiyo mfumo unawapa nafasi moja kwa moja watoto wasio na asili ya kifaransa kuingia kwa wingi kwenye timu ya taifa ya soka ya Ufansa.

Inapofika kwenye hatua kubwa kama hii ya kuteua timu ya taifa unakuta wachezaji wengi wanaoitwa kwenye timu ya taifa ya Ufaransa ni wenye asili ya kiafrika. Kwa mfano unapewa jukumu la kuteua timu ya taifa ya Ufaransa, unamwachaje Paul Pogba, Bacary Sagna unaitaje beki wa pembeni na kumwacha Patrice Evra, kwahiyo mwisho wa siku unakuta mfumo mzima wa mpira wa Ufaransa hususan ngazi ya vijana unawapa nafasi kubwa wachezaji ambao asili yao siyo Ufaransa.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top