Maoni ya Zitto Kabwe kufuatia Kauli za Mrema na Cheyo kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Jana

Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Mjini
Unashangaa ya Mrema ( TLP ) na Cheyo ( UDP )? Kama ni msomaji wa Siasa za Dunia wala hutasumbuka maana NI mambo yamefanyika sana. Hao ndio systemic opposition.
Jambo la muhimu ni kujua kuwa Rais wa sasa sio yule aliyemtangulia na hivyo CCM ya kuanzia Leo haitakuwa CCM iliyoishia Jana. Rais anayeweza kutamka hadharani kuwa ' angewapoteza' watu, tena wanachama wa Chama chake, kwa kuonyesha kutokukubaliana na Maamuzi ya chama ndani ya vikao vya Chama, ni mtu hatari na hivyo mbinu za kushindana naye lazima ziwe tofauti.
Huu ndio wakati wa kujenga Mfumo madhubuti wa Vyama vingi kuliko wakati mwengine wowote katika historia ya Nchi yetu. Nasaha zangu kwa Viongozi wote wa upinzani ni ' tujisomee kwanza '! Tujue mbinu na medani. Pia Sisi tuwe ' more democratic ' kuliko CCM kwa kuruhusu maoni tofauti kwenye Vyama vyetu badala ya kuwa na tabia zile zile za CCM.
Mrema na Cheyo wamekuwa wenyeviti wa Vyama vyao tangu Mwinyi ni Mwenyekiti wa CCM na bado hawaoni haya wala soni kusifia CCM na mfumo wao wa kubadilishana Uongozi. Cheyo alikuwapo Mwinyi alipomkabidhi Mkapa, Mkapa alipomkabidhi Kikwete na Kikwete alipomkabidhi Magufuli! Kote huko alitoa hotuba. Wachambuzi wa Siasa wangechambua hotuba za Cheyo miaka yote hiyo na kumwuliza anajisikiaje!
Uenyekiti wa Magufuli CCM ni faida kwa mfumo wa Vyama vingi kwani Upinzani wa kweli utaimarika. Upinzani wa Hoja na Masuala utaimarika zaidi kuliko wakati mwengine wowote.
Huu ndio wakati wa kusambaza Azimio la Tabora linalohuisha Azimio la Arusha.

Zitto Kabwe's photo.


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top