MANARA, MURO USO KWA USO


MSIBA wa Mwanahabari Elizabeth Mayemba umewakutanisha Maafisa Mawasiliano wa klabu mbili kongwe za Simba na Yanga Jerry Muro na Haji Manara.

Wawili hao walikutana katika shughuli ya kuagwa mwili wa marehemu nyumbani kwake Tabata Kisukulu na kuzima hali ya utofauti wao wakiwa kazini wakilakiana
kwa furaha kisha kuzungumza.

Aliyetangulia kufika msibani hapo alikuwa ni Muro ambapo baadaye Manara akafuata kabla ya Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas kuungana nao na kufanya kikao kifupi.

Watatu hao mara baada ya kumaliza shughuli za kuaga mwili wa marehemu Eliza walikutana nje na kufanya kikao kifupi tukio ambalo liliwashangaza wengi kwa kila mmoja kuamua kuchukua kumbukumbu ya picha yao.

Haikujulikana mara moja walichokuwa wakikijadili katika kikao hicho lakini kila mmoja alionekana kuzungumza kwa msisitizo kama vile ni watu ambao hawana tofauti.
Credit:Dauda

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top