Jukwaa Huru la Wazalendo Lalaani Maamuzi ya Meya wa Dar es salaam

Siku chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kutoa agizo la msako wa nyumba hadi nyumba ili kuwabaini watu wasio na kazi maalum, Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita aliibuka na kudai agizo hilo ni batili na haliwezi kutekelezeka kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Jukwaa Huru la Wazalendo kwa Mkoa wa Dar es Salaam kupitia kwa Mwenyekiti wake Andrew Kadege wamelaani vikali kitendo kilichofanywa na Meya wa Dar es Salaam, Isaya Mwita kwa kufanya harakati za siasa badala ya zile za kuwaletea wananchi maendeleo huku akiwapotosha kwa makusudi wananchi na kuwataka kukaidi agizo la Makonda.

Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania limewataka wananchi wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla kutoa ushirikiano mara zoezi la kuwatambua wakazi katika kaya litakapoanza rasmi ili kupata takwimu sahihi kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla hususan katika kipindi hiki ambapo serikali inataka kuanza ugawaji wa Sh. Milioni 50 kusaidia maendeleo ya kaya.


Hata hivyo jukwaa limemtaka meya kutokuendelea na tabia ya kuwalaghai wanainchi kutoshiriki katika shughuli za maendeleo kwani ndio sehemu yao ya kujikwamua kiuchumi na kuondoa umasikini unaowakabili watanzania kwa ujumla.


Jukwaa limeongeza kuwa hatua hiyo ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ya kutaka kuwatambua wanainchi wa mkoa wake wa Dar es salaam katika ngazi ya kaya ni kutaka kujua jinsi gani ya kuweza kupanga na kuwahudumia kama ilivyo katika majiji ya London,Paris na Berlin inavyofanyika.


Jukwaa huru limechukua nafasi hiyo kuwaomba na kuwashauri wanainchi wote popote litakapo fanyika zoezi hilo kushirikiana na serikali kikamilifu kwani ni kwa manufaa ya wanainchi wenyewe na taifa kwa ujumla ili kuweza kuinua uchumi.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top