Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendelea (CHADEMA) Freeman A Mbowe akiwasilisha maazimio kwa wanahabari leo
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAMATI KUU ILIYOFANYIKA
HOTELI YA BAHARI
BEACH LEDGER PLAZA, 23-26 JULAI, 2016
1.0
UTANGULIZI
Kamati
Kuu ya dharura ya Chama iliketi kuanzia tarehe 23-26 Julai, 2016 Jijini Dar Es
Salaam na ilikuwa na ajenda moja mahsusi ambayo ni kujadili hali ya siasa na
uchumi wa Taifa tangu serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani mwezi
Novemba, 2015.
Mwenendo
wa serikali hii ya CCM ya awamu ya tano, chini ya Rais John Magufuli, ni dhahiri
kuwa umeamua kuiweka demokrasia kizuizini na kuleta utawala wa Kidikteta katika
nchi yetu.
2.0
MATUKIO MAHSUSI
YA UKANDAMIZAJI WA
HAKI NA DEMOKRASIA
NCHINI
2.1
Kupiga
Marufuku Mikutano ya Vyama vya Siasa: Serikali kupitia
Waziri Mkuu na hatimaye Rais na
jeshi la Polisi walitangaza kwa nyakati tofauti kwamba ni marufuku kwa vyama
vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa mpaka mwaka 2020 ili kuipa Serikali
nafasi ya kufanya kazi. Huu ni uvunjaji wa Ibara ya 20 (1) ya Katiba.
Aidha,
katazo la mikutano ya siasa linakiuka Sheria namba 5 ya Vyama vya siasa ya
mwaka 1992 kifungu cha 11 ambayo imetoa haki kwa vyama vya siasa kufanya kazi
ya siasa.
2.2 Kupiga Marufuku Urushwaji wa moja kwa
moja (live coverage) wa Mijadala ya Bunge: Katazo hilo ni
kinyume na Katiba ibara ya 18 ya Jamhuri ya
1
2.3 Kudhibiti Wabunge wa Upinzani Bungeni: Serikali
imejificha nyuma ya kiti cha Naibu
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (Mb) ili kuwadhibiti Wabunge wa
Upinzani Bungeni kwa lengo la kuwanyamazisha wasiikosoe Serikali.
Ikumbukwe
kwamba Dkt. Tulia akiwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa ni mtumishi
wa umma asiyepaswa kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa; lakini ghafla
anaonekana akigombea nafasi ya Naibu Spika kupitia CCM. Hivyo yupo Naibu Spika
ambaye ni mteule wa Rais. Swali: Anawajibika kwa nani kati ya Bunge na Rais?
2.4
Kuingilia
Mhimili wa Mahakama: Serikali ya CCM kupitia Rais, kwa nyakati tofauti imeonekana kujaribu kuingilia
uhuru wa Mahakama jambo ambalo ni hatari kwa utoaji wa haki nchini. Katika
hotuba yake, wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria duniani Rais alinukuliwa
akisema kwamba Mahakama iwahukumu harakaharaka watu waliokwepa kodi halafu
atatumia asilimia fulani ya fedha ambazo zitakuwa zimepatikana kutokana na
faini za wale walioshindwa kesi kuwapa Mahakama.
2.5
Kupuuza
Utawala wa Sheria: Tarehe 24 Juni, 2016 wakati wa uzinduzi wa
siku ya usalama wa raia, Rais
Magufuli alinukuliwa akiwaruhusu polisi kuwaua majambazi bila kuwafikisha
mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. Aidha aliuagiza uongozi wa Jeshi la
Polisi kuwapandisha vyeo watakaowauwa majambazi.
2.6
Muswada
wa Sheria ya Haki ya kupata habari –Serikali imepeleka
Bungeni Muswada wa Sheria ya Haki ya
kupata habari. Sheria hii imeweka adhabu kubwa sana kwa waandishi kama vile
kifungo cha miaka 15 na kisichozidi miaka 20 kwa mujibu wa kifungu cha 6(6)
2
Tangu
serikali ilipoingia madarakani hali ya ukuaji wa uchumi na hata uwekezaji wa
mitaji imekuwa ikiporomoka kwa kasi kubwa sana nchini mwetu na hata baadhi ya
wawekezaji wanaondoa mitaji yao kutokana na serikali hii kukosa mwelekeo
unaoeleweka wa Kiuchumi.
2.8
Serikali za mitaa
kunyanganywa mapato na serikali kuu.
Baada
ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 tulifanikiwa kushinda maeneo ya Majiji ya DSM,
Mbeya,Arusha na Miji mikubwa ya Iringa, Moshi,Bukoba,Babati,Tunduma na
mingineyo ya maeneo ya mijini ambayo kwa kiasi kikubwa wanategemea sana
kuendesha Halimashauri hizo kwa kutumia kodi ya Majengo Kodi ya Majengo
inachangia kati ya 30% hadi 60% ya mapato ya ndani ya Mamlaka za Miji.
2.9
Diplomasia na mahusiano ya kimataifa
Hivi karibuni serikali imetoa maelekezo kupitia mawasiliano yake na
Mabalozi (Note Verbale) kuelekeza kuwa kabla ya Mabalozi au maofisa wa Ubalozi
kukutana na asasi zisizo za
kiserikali au vyama vya siasa ni lazima kwanza waombe kibali cha serikali
kupitia Wizara ya Mambo Nje.
Utaratibu
huu unaminya uhuru wa mabalozi na wanadiplomasia mbalimbali kufanya kazi zao
nchini na ni utaratibu ambao unakiuka utamaduni uliokuwepo awali na pia
unakiuka masharti ya Mkataba wa Vienna kuhusu mahusiano ya Kibalozi Duniani.
2.10
Uteuzi wa Wakurugenzi wa Halimashauri
Uteuzi wa Rais wa Wakurugenzi wa Halimashauri na Makatibu Tawala wa
Wilaya haukuzingatia sheria za utumishi wa umma na badala yake umezingatia
kigezo cha Ukada zaidi badala ya weledi na historia katika utumishi wa umma
kama ambavyo sheria zinataka, zaidi ya wakurugenzi 80 na Makatibu tawala zaidi
ya 40 waligombea kura za maoni ndani ya CCM 2015.
2.11
ZANZIBAR
Kwa sababu ya hasira ya kukataliwa kwa CCM, vikosi vya ulinzi na hasa
Jeshi la Polisi vimekuwa vikishiriki katika vitendo kadhaa vya ukiukwaji wa
haki za raia huko Zanzibar ambapo kwa zaidi ya miezi miwili sasa, wamekuwa
wakipita katika vijiji na kuwapiga, kuwatesa, kuwakamata, kuwatishia na hata
kuharibu mali za wananchi na mifugo yao
3
Tunawataka
wananchi wa Unguja na Pemba waendelee kuikataa Serikali haramu iliyopo
madarakani huko Zanzibar kwa njia za amani .
3.0
MAAZIMIO YA KAMATI KUU
Baada ya majadiliano Kamati Kuu imeazimia
ifuatavyo;
3.1
Septemba 1, siku ya
mikutano ya hadhara nchi nzima
Kamati
kuu imeagiza ngazi zote za chama kuanzia ngazi ya msingi, Kata, Majimbo,
Wilaya, Mikoa, Kanda, Mabaraza na Taifa kukaa vikao vyake vya kikatiba na
imeelekeza ajenda ya vikao hivyo kuwa ni kujadili hali ya siasa, hali ya uchumi
na maandalizi ya mikutano ya hadhara ya tarehe 01 Septemba, 2016 nchi nzima.
3.2
Wanasheria wa Chama
kuchukua hatua
Kamati Kuu imewataka
wanasheria wa chama kukaa na kuyatazama mambo yote ambayo yametokea na kuchukua
hatua za kisheria kwa lengo la kuyatafutia suluhisho la kisheria.
3.3
OPERESHENI UKUTA
UMOJA
WA KUPAMBANA NA UDIKTETA TANZANIA (UKUTA)
UTANGULIZI
Kwa
mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika utangulizi kuna
maneno yameandikwa na ambayo yamekaziwa na sheria namba 15 ya mwaka 1984 ibara
ya 3 na sheria namba 1 ya mwaka 2005 ibara ya 3. Katika utangulizi huo wa
katiba yetu imeandikwa kama ifuatayavyo;
“KWA
KUWA Sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa
dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki,
udugu na amani”
4
“NA
KWA KUWA misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia, ambayo Serikali yake
husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi
na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala
upendeleo wowote na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa
na kulindwa na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu:”
“KWA
HIYO, BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGE MAALUM LA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA kwa niaba ya Wananchi kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo na pia
kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata
misingi ya Demokrasia ujamaa na
isiyokuwa na Dini”
Aidha
kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzana ibara ya 3 (1) inasema
kuwa “Jamhuri ya Muungano ni Nchi ya Kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na
dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa”
Ni
wazi sasa kuwa kuna tishio kubwa dhidi ya ukuaji wa Demokrasia hapa Nchini
mwetu kutoka kwa viongozi wa serikali hii ya awamu ya tano kukandamiza Demokrasia
na madhara ya kukandamizwa kwa demokrasia yameshaanza kulitafuna taifa letu.
Ni
dhahiri kuwa kama raia wema tuna wajibu na haki ya kuilinda na kuitetea Katiba
ya Nchi na kuhakikisha kuwa haivunji na yeyote na misingi ya Kidemokrasia ambayo ilijengwa kwa
miongo mingi inaendelea kuimarika, kulelewa na kukuzwa mara dufu.
3.
4 KWANINI UKUTA NI MUHIMU !
Wakati
wa Ufashisti wa Adolf Hitler huko Ujerumani unaanza kuchipua kabla ya kukomaa
alianza kuchukua hatua mbalimbali za kuwanyamazisha Wajerumani kwa njia
mbalimbali ili aweze kutawala kwa mkono wa Chuma.
Alikuwepo
Mchungaji mmoja anayejulikana kwa jina la Martin
Niemoller na ambaye alikuwa akimsemea Hitler kwa kila hatua ambazo alikuwa
anachukua dhidi ya makundi mengine katika jamii ya wajerumani bila kujua kuwa
lilikuwa ni suala la muda tu kabla hata yeye hajafikiwa na mkono wa Chuma wa
Hitler.
Mchungaji
huyu ni maarufu sana kwa msemo wake ambao aliutoa alipofikiwa na mkono wa
Hitler ambao ulimpelekea kuishia jela kwa miaka 7 na wakati huo hapakuwa na
mtetezi wa kumsemea,
alisema hivi;
5
they
|
came
|
for
|
the
|
Socialists,
|
and
|
I
|
did
|
not
|
speak
|
out—
|
|
Because I was not a Socialist.
|
|||||||||||
Then
|
they
|
came
for the Trade
Unionists,
|
and
|
I did
|
not
|
speak
|
out—
|
||||
Because
I was not a Trade Unionist.
|
|||||||||||
Then
|
they
|
came
|
for
|
the
|
Jews,
|
and
|
I
|
did
|
not
|
speak
|
out—
|
Because
I was not a Jew.
|
Then
they came for me—and there was no one left to speak for me.
3.5
HALI TANZANIA IKOJE?
Tangu
utawala wa awamu ya Tano ulipoingia madarakani mwezi Novemba, 2015 umechukua
hatua mbalimbali za kubinya Demokrasia na kuua dhana ya utawala bora kwa njia
mbalimbali.
Yapo
makundi ya kijamii ambayo tayari yameshaumizwa au kubinywa na watanzania walio
wengi wanakaa kimya kwa sababu wao sio sehemu ya kundi husika ambalo limenyimwa
haki au kwa kuwa hajafikiwa moja kwa moja.
3.6 KWANINI NI MUHIMU KUJENGA UKUTA.
·
Rais alipiga marufuku safari za nje kwa
watumishi wa umma- sikusema kwa kuwa mimi sikuwa mtumishi wa umma
·
Rais aliitaka mahakama kuu iwahukumu
wafanyabiashara ambao wana kesi za kodi na serikali lazima ishinde-sikusema kwa
kuwa sikuwa mfanyabiashara na wala sikuwa na kesi ya kodi
·
Serikali iliingilia Bunge na kupanga kamati
za kudumu za Bunge-sikusema kwa kuwa mimi sikuwa mjumbe
·
Serikali ilizuia matangazo ya Bunge live-sikusema
kwa kuwa mimi sio Mbunge
·
Wabunge wa Upinzani kunyanyaswa Bungeni na
kuonewa –sikusema kwa kuwa mimi sio UKAWA
·
Hotuba za Upinzani kufutwa Bungeni kinyume
cha Kanuni za Bunge –sikuwa mpinzani nilikaa kimya
·
Bunge kurejesha fedha zake kwa Rais kinyume
cha sheria –sikusema kwa kuwa halinihusu
·
Tume ya Taifa ya Uchaguzi kurejesha fedha
kwa Rais kinyume cha sheria – sikusema kwa kuwa Tume hainihusu
6
·
Serikali Kuwafukuza na kuwadhalilisha
wanafunzi wa UDOM –sikusema kwa kuwa sina ndugu wala mtoto anayesoma UDOM.
·
Mikutano ya kisiasa kupigwa Marufuku –sikusema kwa
kuwa mimi sio mwanasiasa
·
Wafanyabiashara kupelekewa bili kubwa za
kodi na hata kuzuiliwa kwa Akaunti zao-sikusema kwa kuwa mimi sio
mfanyabiashara
·
Uchumi unaporomoka kwenye sekta zote nchini
-sikusema kwa kuwa mimi sijawahi kumiliki uchumi
·
Fao la kujitoa limeondolewa kwenye Mifuko ya
hifadhi ya jamii, sikusema kwa sababu mimi si mwanachama wa mifuko ya hifadhi
ya jamii.
·
Mashirika na Makampuni kuanza kupunguza
wafanyakazi kutokana na kuporomoka kwa uchumi –sikusema kwa kuwa sijapunguzwa
kazini
·
Mabalozi na wanadiplomasia kuzuiliwa
kukutana na viongozi wa kisiasa bila kibali cha serikali- sikusema kwa kuwa
halinihusu
·
Watumishi wa umma kulazimishwa kwenda
kinyume na sheria na kanuni za utumishi wa umma wametakiwa kuwa Makada wa CCM –sikusema
kwa kuwa mimi sio mtumishi wa umma
·
Ukaguzi wa vyeti vya kidato cha nne na
kutumika kama msingi wa kufukuza watu kazi hata kama ni Maprofesa –sikusema kwa
kuwa hawajaja kwenye sekta yangu
·
Watumishi wa umma kutumbuliwa majipu bila
kufuatwa kwa sheria na kanuni za utumishi wa umma –sikusema kwa kuwa mimi
sikutumbuliwa
·
Mawakili kuunganishwa kwenye kesi za wateja
wao wanapoenda kuwatetea – sikusema kwa kuwa mimi sio wakili
·
Waalimu kukatwa mishahara iwapo dawati
litavunjika kwenye shule yake – sikusema kwa kuwa mimi sio mwalimu
·
Kupotezwa kwa wana CCM ambao watapinga kauli
ya Mwenyekiti au kuwa na maoni tofauti-sikusema kwa kuwa mimi sio mjumbe wa
vikao vya CCM .
·
Muswada wa sheria ya haki ya kupata habari
na adhabu ya kifungo cha miaka 15-20- sikusema kwa kuwa mimi sio mwandishi wa
habari
·
Viongozi wa dini kudhalilishwa –sikusema kwa kuwa
mimi sio kiongozi wa dini
·
Unyanyasaji na udhalilishaji wa wananchi
Zanzibar –sikusema kwa kuwa mimi sio mzanzibari
3.7
TUCHUKUE HATUA!
i.
Kwa kuwa wewe tayari umeshafikiwa hauna budi
kujenga UKUTA ili kuzuia wengine
wasidhurike na utawala huu.
ii.
Kwa kuwa wewe hujafikiwa na ndio maana
husemi wenzako wanapofikiwa, njoo tujenge UKUTA
ili ukifikiwa awepo wa kusema
7
iv.
Njoo Tujenge UKUTA
kuzuia Udikteta huu
v.
Tujenge UKUTA
tuilinde Katiba yetu
vi.
UKUTA
huu ni wa wananchi wote bila kujali dini, kabila, chama cha siasa au rangi
Historia
inaonyesha kuwa Duniani pote Hakuna utawala uliwahi kuushinda UKUTA wa wananchi .Na hii ndio Nguvu ya
Umma. Kila mmoja achukue hatua popote alipo ya kujenga UKUTA!
Imetolewa
na;
…………………….
Freeman
A Mbowe
Mwenyekiti
wa CHADEMA Taifa
27
Julai, 2016
Haya hapa majina 1,091 ya wadaiwa yaliyotangazwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu bofya hapa
Breaking News: IRINGA: Askari aliyemuua mwanahabari Daudi Mwangosi ahukumiwa kufungwa Jela bofya hapa
Breaking news: Ajali mbaya ya Basi la UDA lagonga Treni Kariakoo,Mmoja Afariki, 45 Wajeruhiwa bofya hapa
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano July 27, 2016 bofya hapaNAFASI ZA KAZI BOFYA HAPA
TCU yakanusha taarifa za kuvifungia udahili wa kozi tofauti vyuo 22 zilizozagaa juzi bofya hapa
Tume ya vyuo Vikuu Tanzania( TCU) yatangaza vyuo Vikuu vilivyofungiwa BOFYA HAPA
News alet:Majina ya wanafunzi waliochanguliwa kujiunga Certificate na Diploma na NACTE 2016/2017 bofya hapa
News alert:Tume ya vyuo Vikuu Tanzania( TCU) yatangaza vyuo Vikuu vilivyofungiwa BOFYA HAPA
Orodha ya majina ya wanchuo watakaorudi kusoma Udom bofya hapa
Matokeo ya form six 2016 bofya hapa
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
Breaking news: Ajali mbaya ya Basi la UDA lagonga Treni Kariakoo,Mmoja Afariki, 45 Wajeruhiwa bofya hapa
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano July 27, 2016 bofya hapaNAFASI ZA KAZI BOFYA HAPA
TCU yakanusha taarifa za kuvifungia udahili wa kozi tofauti vyuo 22 zilizozagaa juzi bofya hapa
Tume ya vyuo Vikuu Tanzania( TCU) yatangaza vyuo Vikuu vilivyofungiwa BOFYA HAPA
News alet:Majina ya wanafunzi waliochanguliwa kujiunga Certificate na Diploma na NACTE 2016/2017 bofya hapa
News alert:Tume ya vyuo Vikuu Tanzania( TCU) yatangaza vyuo Vikuu vilivyofungiwa BOFYA HAPA
Orodha ya majina ya wanchuo watakaorudi kusoma Udom bofya hapa
Matokeo ya form six 2016 bofya hapa
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
Breaking News: IRINGA: Askari aliyemuua mwanahabari Daudi Mwangosi ahukumiwa kufungwa Jela bofya hapa
Breaking news: Ajali mbaya ya Basi la UDA lagonga Treni Kariakoo,Mmoja Afariki, 45 Wajeruhiwa bofya hapa
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano July 27, 2016 bofya hapaNAFASI ZA KAZI BOFYA HAPA
TCU yakanusha taarifa za kuvifungia udahili wa kozi tofauti vyuo 22 zilizozagaa juzi bofya hapa
Tume ya vyuo Vikuu Tanzania( TCU) yatangaza vyuo Vikuu vilivyofungiwa BOFYA HAPA
News alet:Majina ya wanafunzi waliochanguliwa kujiunga Certificate na Diploma na NACTE 2016/2017 bofya hapa
News alert:Tume ya vyuo Vikuu Tanzania( TCU) yatangaza vyuo Vikuu vilivyofungiwa BOFYA HAPA
Orodha ya majina ya wanchuo watakaorudi kusoma Udom bofya hapa
Matokeo ya form six 2016 bofya hapa
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
Breaking news: Ajali mbaya ya Basi la UDA lagonga Treni Kariakoo,Mmoja Afariki, 45 Wajeruhiwa bofya hapa
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano July 27, 2016 bofya hapaNAFASI ZA KAZI BOFYA HAPA
TCU yakanusha taarifa za kuvifungia udahili wa kozi tofauti vyuo 22 zilizozagaa juzi bofya hapa
Tume ya vyuo Vikuu Tanzania( TCU) yatangaza vyuo Vikuu vilivyofungiwa BOFYA HAPA
News alet:Majina ya wanafunzi waliochanguliwa kujiunga Certificate na Diploma na NACTE 2016/2017 bofya hapa
News alert:Tume ya vyuo Vikuu Tanzania( TCU) yatangaza vyuo Vikuu vilivyofungiwa BOFYA HAPA
Orodha ya majina ya wanchuo watakaorudi kusoma Udom bofya hapa
Matokeo ya form six 2016 bofya hapa
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)