Euro 2016:Kwa rekodi hivi za hivi karibuni Ureno atachomoka kweli, Je atalipa kisasi fainali ya Leo?

Timu ya taifa ya Ureno huenda ikapata nafasi nzuri ya kulipiza kisasi baada ya kufanikiwa kucheza fainali ya Euro 2016 dhidi ya timu wenyeji Ufaransa, ambaye mara kadhaa imekuwa ikipata ushindi inapocheza na Ureno
.
Fainali hiyo inatarajiwa kuchezwa Leo katika uwanja wa Stade  de France uliopo Paris, Ufaransa, Huenda ikawa mechi ya aina yake inayozikutanisha timu hizo mbili zenye histori atofauti. Ureno imewahi kupoteza michezo 10 ya kimataifa iliyocheza dhidi ya Urafansa hivi karibuni hivyo fainali hii inaweza kuwa nafasi nzuri kwa Ureno kurekebisha Makosa  katika michezo iliyopita na Kuilaza Ufaransa. kwa upande mwingine Ufaransa inaweza kuendeleza ubabe dhidi ya Ureno.
Ikumbukwe majuzi nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo kuifunga Wales mabao 2-0 huku Ufaransa ikiilaza Ujerumani 2-0.
Zaidi ya Miongo Minne iliyopita baada ya mchezo wa kirafiki ambao Ufaransa ilishinda 2-0 wakati Marius Tresor akiwa miongoni mwa wachezaji wa Ufaransa.Ureno haijafanikiwa kuwafunga wapinzania wao Ufaransa.
Ureno inafahamu ukweli kuwa ina kibarua kigumu baada ya kufungwa michezo kumi ikiwemo mchezo wa nusu fainali ya Euro 2000 na nusu fainali ya Kombe la Dunia ya 2006.
Mchuano mwingine Mkubwa ambao ulizikutanisha timu hizo ni Euro 1984 katika nusu fainali ambapo Ureno ilipoteza Dhidi ya Ufaransa.
Lakini Ronaldo kwa kujiamini anasema wanaweza kurudi nyumbani na Kombe hilo baada ya kuwafunga wapinzani wao Ufaransa. 

 Ikilinganishwa fainali hii na ile ambayo Ureno ilipoteza dhidi ya Ufiriki miaka 12 iliyopitaRonaldo anasema kuna tofauti kubwa sana wakati huo Ronaldo alikuwa na miaka 19 tu ambapo kwa sasa ana miaka 31.
Ronaldo anadai kwamba licha ya kufungwa katika michezo yote hiyo kwa sasa ni wakati wao wa kujiuliza na kuifunga Ufaransa kama ambavyo awao walifungwa katika michezo iliyopita.
Lakini kwa Upande wa Shujaa wa Ufaransa, Antoine Griezmann amepingana na Ronaldo kwa madai kuwa kiwango walichokionyesha dhidi ya Ujerumani ni kielezo tosha cha ushindi dhidi ya Ureno. Ambapo mabao mawili aliyofunga katika mchezo huo yalitosha kuwasambaratisha Ujerumani ambao ni mabingwa wa kombe la Dunia 2014 na kurudi kwao vichwa chini.


 Tujikumbushe rekodi na mabao katika mechi ambazo Ureno walikutana na Ufaransa

March 8, 1978 Ufaransa 2-0 Ureno (Kirafiki)

Feb 16, 1983  Ureno 0-3 Ufaransa (Kirafiuki)

Jun 23, 1984 Ufaransa 3-2 Ureno (Euro)

Jan 24, 1996 Ufaransa 3-2 Ureno (Kirafiki)

Jan 22, 1997 Ureno 0-2 Ufaransa (Kirafiki)

Jun 28, 2000 Ufaransa 2-1 Ureno (Euro)

April 25, 2001 Ufaransa 4-0 Ureno (Kirafiki)

July 5, 2006 Ufaransa 1-0 Ureno (Kombe la Dunia)

Oct 11, 2014 Ufaransa 2-1 Ureno (Kirafiki)

Sept 4, 2015 Ureno 0-1 Ufaransa (Kirafiki)

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top