Cruz azomewa kwa kutomuunga mkono Trump

Cruz amesema anataka maadili ya Republican yashindee

Wajumbe katika kongamano kuu la chama cha Republican nchini Marekani wamemzomea seneta wa Texas, Ted Cruz, baada yake kukosa kumuidhinisha Donald Trump kuwa mgombea wa chama hicho.

Bw Cruz alikuwa amesalia kuwa mpinzani pekee wa Bw Trump lakini akajiondoa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mchujo jimbo la Indiana mapema mwezi Mei.

Bw Cruz, akihutubu katika kongamano hilo linalotumiwa kuamua mgombea wa chama hicho kwenye uchaguzi mkuu Novemba, amesema tu kwamba anataka maadili ya chama cha Republican yashindwe kwenye uchaguzi huo.
Waandishi wa habari wanasema hatua ya Bw Cruz kukataa kumuunga mkono wazi bw Trump inatokana na migawanyiko ambayo imeendelea katika chama hicho kuhusu ugombea wa Bw Trump.

Gavana wa Indiana Mike Pence alikubali rasmi kuwa mgombea mwenza wa Bw Trump kwenye kongamano hilo.

Ameeleza maadili yake ya kihafidhina na akashambulia maadili na historia na sifa za Hillary Clinton, mgombea wa chama cha Democratic.

Baada yake kumshutumu Bi Clinton, wajumbe wamerudia kuimba "Lock Her Up" (Afungwe) kwa siku ya tatu mfululizo.

Bw Trump anatarajiwa kuhutubia kongamano hilo Jumatano.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top