Chadema kutoa tamko zito Leo Ambalo Litarushwa na Vituo Vitatu vya TV

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), leo kinatarajia kulihutubia taifa kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje kuhusu maazimio ya Kamati Kuu iliyoketi kwa siku nne mfululizo
.
Maazimio hayo ambayo yanaitwa ‘mazito na makubwa’ kuwahi kutolewa na chama hicho katika siku za hivi karibuni, yanatarajiwa kuonyeshwa moja kwa moja na vituo vitatu vya runinga nchini.


Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya chama hicho kimeeleza kuwa maazimio hayo ya Kamati Kuu yatatangazwa moja kwa moja kupitia baadhi ya vituo vya runinga kutoa fursa kwa Watanzania kusikiliza maazimio hayo.


Kamati kuu ya Chadema imefanya kikao chake kwa siku nne mfululizo kikiwa kimeghubikwa na usiri mkubwa.


Taarifa ya chama hicho kwa vyombo vya habari jana, ilisema Kamati Kuu ilimaliza kikao chake cha siku nne jana na leo maazimio yake yatawekwa wazi kwa wananchi kupitia vyombo vya habari.


Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene, ilisema kupitia mkutano huo yatatangazwa maazimio ya kikao hicho kilichohitimishwa Dar es Salaam jana.


Taarifa hiyo ilisema Chadema kitatoa tamko zito la ukubwa wa aina yake.


“Licha ya mambo hayo chama kitatoa matamko mazito na makubwa ya aina yake ambayo hayajawahi kutolewa na chama chetu katika siku za karibuni."


Taarifa hiyo ilisema Kamati Kuu ilipokea taarifa ya kina juu ya masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na hali ya siasa nchini kwa sasa ambayo inatishia hali ya uchumi na ustawi wa jamii nzima kwa ujumla, hivyo taifa zima kuwa katika majaribu makubwa ya kukosa mwelekeo wa uongozi.


“Kupitia mkutano huo, Chadema kitatoa mwelekeo wa hali ya nchi hasa wakati huu ambao taifa linaonekana kukosa dira ya uongozi kwa ajili ya ustawi wa Watanzania wote kwa ujumla” kilisema chanzo hicho ambacho hakikutaka kuwekwa wazi jina lake.


“Kupitia mkutano huo, chama kitazungumzia mipango ya kujiimarisha kuendelea kuwatumikia wananchi na kusimamia dira ya mabadiliko na uhuru wa kweli nchini,”alisema Makene.


Alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, Makene alisema suala hilo halijathibitishwa rasmi kama mkutano huo utaonyeshwa moja kwa moja katika runinga. 
Mkutano wa Chadema leo na Wanahabari, Mbowe atangaza maazimio mazito bofya hapa 


“Hata mahali utakapofanyika mkutano huo bado hapajajulikana, nitakupigia simu kesho asubuhi (leo) kukujulisha wapi tamko hilo litatolewa." Alisema
 Breaking news: Ajali mbaya ya Basi la UDA lagonga Treni Kariakoo,Mmoja Afariki, 45 Wajeruhiwa bofya hapa

 Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano July 27, 2016 bofya hapaNAFASI  ZA KAZI BOFYA HAPA 



Tume ya vyuo Vikuu Tanzania( TCU) yatangaza vyuo Vikuu vilivyofungiwa BOFYA HAPA


News alet:Majina ya wanafunzi waliochanguliwa kujiunga Certificate na Diploma na NACTE 2016/2017 bofya hapa

News alert:Tume ya vyuo Vikuu Tanzania( TCU) yatangaza vyuo Vikuu vilivyofungiwa BOFYA HAPA
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top