Mshambuliaji raia wa Zambia Obrey Chirwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea klabu ya Yanga.
Chirwa ambaye alikuwa anaichezea klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe, amewasili leo jioni jijini
Dar na kukamilisha taratibu za usali na sasa Yanga imeshakamilisha idadi ya wachezaji saba wa kimataifa kwa mujibu wa kanuni na sheria za TFF.
Nyota huyo anaungana na wachezaji wengine waliowahi kuichezea FC Platinum Donald Ngoma na Thaban Kamusoko ambao walisajiliwa msimu uliopita.
Klabu ya FC Platinum imethibitisha pia nyota huyo kujiunga na Yanga kwa kuandika ujumbe kwenye akaunti rasmi ya klabu hiyo uliosomeka: “Obreu Chirwa amejiunga rasmi na klabu ya Young Africans ya Tanzania kwa mkataba wa muda mrefu. Kila laheri kwenye safari yako mpya,” huo ni ujumbe ulioandikwa na klabu ya Chirwa.
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA