Kiongozi wa chama cha UKIP Nigel Farage akisherehekea ushindi wao
Asilimia kubwa ya raia wa Uingereza wamepiga kura ya maoni wakiitaka ijiondoe kwenye muungano wa bara Ulaya EU.
Huku asilimia kubwa ya kura zikiwa zimekwisha hesabiwa, asilimia 52% ya raia wa Uingereza wamepiga kura ya kumaliza uanachama wa Uingereza ndani ya EU uliodumu miaka 43.Watu wanaoishi katika mji London na Scotland ndio waliopiga kura kwa wingi kusalia ndani ya muungano huo.
Huko Wales wapiga kura 854,572 (52.5%) waliamua kujiondoa huku wengine 772,347 (47.5%) wakipiga kura kusalia katika muungano huo.
Watu wanaoishi katika mji London na Scotland ndio waliopiga kura kwa wingi kusalia ndani ya muungano huo.
Msemaji wa chama cha Wales Conservatives na mmoja wa wanaharakati wakuu wa kujiondoa Uingereza Andrew RT Davies anasema kuwa kuanzia leo siasa za Wales zimebadilika kabisa.Kati ya maeneno 17 ya uwakilishi nchini Wales maeneo 5 pekee ndio yaliyopiga kura ya kutaka kusalia kwenye muungano huo.
Wapinzani wao hata hivyo wanadai kuwa Uingereza sasa imeingia katika awamu yenye misukosuko ya kiuchumi na kisiasa.
Kati ya maeneno 17 ya uwakilishi nchini Wales maeneo 5 pekee ndio yaliyopiga kura ya kutaka kusalia kwenye muungano huo.
Maeneo ya uwakilishi ya Gwynedd, Cardiff, Ceredigion, the Vale of Glamorgan na Monmouthshire ndio yalitaka kusalia kwenye mwavuli huo uliodumu kwa miaka 43.
Magufuli: Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Pumzika Kwa Amani, Wewe upo Salama, Usisikilize kelele za Nje Bofya hapa
Vibonzo Katuni tano bora zaidi leo Ijumaa June 24, 2016 Bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
Vibonzo Katuni tano bora zaidi leo Ijumaa June 24, 2016 Bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA