Video: RONALDO ALIMNYIMA JEZI NAHODHA WA ICELAND

Nahodha wa Iceland Aron Gunnarsson anajivunia kuliongoza taifa lake kupata sare ya kufungana bao 1-1 na Ureno, na kupata pointi moja kwenye mashindano ya Ulaya waliyoshiriki kwa mara ya
kwanza.

Lakini baada ya mchezo huo kumalizika, badala ya kwenda kwa mashabiki kuwashukuru kwa sapoti yao na mafanikio wanayopata, Gunnarsson alifikiria kitu ambacho kinaweza kikampa kumbukumbu na ndipo alimfuata Cristiano Ronaldo na kuomba wabadilishane jezi.

Ilimchukua Gunnarsson kama dakika moja au mbili hivi kumfanya Ronaldo ashtuke kama kulikuwa kunamtu anamsemesha. Muda wote wakati akitafuta mbinu ya kuomba jezi ya Ronaldo, nyota huyo wa Real Madrid hakushtushwa na ombi la nahodha wa Iceland.

Angalia video nahodha wa Iceland akimwomba  jezi ya Ronaldo
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top