Uhusiano wa kifedha kati ya UK na EU kuzorota

                                 
                                  Sarafu za Euro

Rais wa nchi za Umoja wa Ulaya wanaotumia sarafu ya Euro, Jeroen Dijsselbloem, amesema sasa taasisi za kifedha za Uingereza zitakuwa na mahusiano machache tu na zile za kifedha za Muungano wa Ulaya baada ya taifa hilo kuondoka rasmi kutoka kwa jumuiya hiyo.

Bw. Dijsselbloem amekiambia kituo cha televisheni cha Uholanzi kuwa hali hiyo itayalazimu baadhi ya makampuni kuhama mji wa London.

Waziri wa fedha wa Uholanzi kwa upande wake amesema anatarajia miji ya Frankfurt na Amsterdam kufaidika kibiashara kutokana na msukumo huo utakaojiri wa biashara kulazimika kuhamia kwengineko Ulaya ili kutoroka masharti magumu ya kazi yatakayoikumba Uingereza baada kujitoa kutoka EU.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top