Ripoti ya sakata la mkataba wa kampuni ya Lugumi Enteprises na Jeshi la Polisi, ambayo ilikuwa iwasilishwe kwenye mkutano unaoendelea wa
Bunge, sasa itawasilishwa kwenye mkutano ujao.
Bunge, sasa itawasilishwa kwenye mkutano ujao.
Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Hilary Aeshi alisema ripoti hiyo itaunganishwa katika taarifa za kamati ambazo kwa utaratibu huwasilishwa kwenye mkutano huo.
Sakata hilo linahusisha utekelezaji mbovu wa mkataba wa kufunga mashine za kielektroniki za kuchukulia alama za vidole kwenye vituo 108 vya polisi.
Hadi wakati Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akifanya ukaguzi wa mkataba huo wa Sh37 bilioni uliosainiwa mwaka 2013, ni vituo 14 tu vilivyokuwa vimefungwa mashine hizo, lakini mzabuni alishalipwa Sh36 bilioni.
Baada ya sakata hilo kuibuliwa, wabunge walitaka liwasilishwe kwenye mkutano unaoendelea mjini Dodoma, lakini PAC ikaunda kamati ndogo ambayo sasa inatakiwa iwasilishe ripoti ya uchunguzi wake.
Hadi jana asubuhi ripoti ya kamati hiyo ndogo, iliyoundwa na wajumbe tisa, ilikuwa bado haijawasilisha ripoti yao.
Hata hivyo, Aeshi ambaye pia ni mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM), alisema alitarajia kukabidhiwa ripoti hiyo na kamati ndogo jana na baada ya hapo kazi ya uchambuzi wa kamati nzima itaanza.
Vibonzo:Katuni tano bora zaidi leo Jumatano June 29, 2016 Bofya hapa
Breaking news: Rais Magufuli ateua Wakuu wa Wilaya na kufanya mabadiliko kidogo ya wakuu wa mikoa bofya hapa
Breaking news: Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameteua wakuu wa wilaya 139, na amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa mikoa Bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA