SIMBA YAKAMATA KIFAA CHA MTIBWA SUGAR

Matukio matatu tofauti wakati Mohamed Ibrahim akisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Simba SC mbele ya Rais wa klabu hiyo
Evans Aveva
Simba SC imemsajilki kiungo Mohamed Ibrahim kutoka klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa mkataba wa miaka miwili kukitumikia kikosi cha Msimbazi huku ada ya uhamisho wake ikiachwa kuwa siri.

Mohamed Ibrahim anakuwa mchezaji wan ne kusajiliwa Simba msimu huu akitanguliwa na nyota mwingine kutoka Mtibwa Sugar Muzamir Yassin nja wachezaji wengine wawili kutoka Mwadui FC Jamal Mnyate kutoka na Emanuel Semwanza.

Simba bado inamnyatia Shiza Kichuya mchezaji mwingine kutoka Mtibwa Sugar ambaye bado mazungumzo ya kuinasa saini yake yanaendelea.

Endapo Kichuya atatua Simba atakuwa ni mchezaji wa tatu kutoka Mtibwa kuhamia Simba msimu huu wakati Mtibwa itakuwa imeuza wachezaji wanne kwenda kwenye vilabu vya Simba na Yanga baada ya Andrew Vicent kusajiliwa Yanga mapema mwezi huu.
Credit:Dauda
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top