HILI NDIYO LILIKUWA JIBU LA RONALDO KWA NAHODHA WA ICELAND AYEOMBA JEZI

Kwa takriban siku nne hivi, kumekuwa na habari picha inayotrend juu ya Cristiano Ronaldo kukataa kubadilishana jezi na nahodha wa Iceland Aron Gunnarsson, punde tu baada ya mwamuzi kupiga filimbi ya kumaliza mchezo.

Baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa, Ronaldo alimwambia Gunnarsson ‘wewe ni nani’ wakati alipokuwa akimtaka wabadilishane jezi.

Sasa issue iko hivi…nahodha huyo wa Iceland jana ameongea na wanahabari na kuweka kila kitu wazi juu ya suala hilo.

Gunnarsson amesema: “Ni kweli kwamba nilimuomba jezi yake, lakini hakuniuliza eti mimi ni nani. Yeye alisema kwamba hakuna tatizo, ila nitakupa tukifika kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Mimi tayari nimeshachoshwa na habari hizi, nataka kuelekeza mawazo yangu yote kwenye mashindano haya, na sidhani kama nina ya kusema zaidi juu ya suala hili.”
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top