Ray C apelekwa sober house Bagamoyo, uongozi wa sober wazungumzia

Muimbaji mkongwe wa muziki nchini, Rehema Chalamila ‘Ray C’ Ijumaa alipelekwa Life and Hope & Rehabilitation Centre (Sober House) iliyopo Bagamoyo kwa ajili ya kusaidiwa kuanacha na matumizi ya Madawa ya kulevya, uongozi wa sober hiyo umethibitisha.


Hatua hiyo imekuja ikiwa ni chache toka aonekane katika video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikionyesha jinsi anavyosaidiwa na jeshi la polisi baada ya kudaiwa kutaka kijichoma kisu.


Mmoja kati ya wasimamizi wa kituo cha Life and Hope & Rehabilitation Centre (Sober House) ambacho pia kilimsaidia Chidi Benz kuachana na matuzi ya Madawa ya kulevya, Karim Banji, amesema kuwa ni siku moja toka Ray C apelekwe katika kituo hicho.


“Kweli jana tumempokea Ray C, na kusema kweli kwa sasa siwezi zungumzia maendeleo yake kwa sababu ni siku ya kwanza, lakini leo mchana amekula vizuri na nimemuacha amepumzika,” alisema Karim.


Pia alisema bado hajajua Ray C atakaa kwa muda gani ndani ya sober house.


“Kusema kweli mgonjwa akiletwa hapa, atapimwa afya na baada ya hapo anawekwa katika chumba maalum kwa siku tatu ili aweze kukabiliana na hali ngumu, na baada ya hapo ataendelea na matibabu ya kawaida, kwa hiyo kikubwa ni kuombea tu,” alisema Karim.
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top