Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe amezitaja kero nyingi alizoziacha Rais Mstaafu Kikwete, ''Kikwete umeniachia mzigo kweli kila sehemu matatizo''alisema Rais Magufuli. Alitaja matatizo ambayo ameyakuta na kuongeza kusema kila sehemu hewa, barabara hewa, wanafunzi hewa, wafanyakazi hewa, ndio maana serikali yake inasimamia sheria kwa nguvu zote.hayo amesema leo mbele ya Rais mstafu Kikwete ambaye ni Mkuu wa chuo Kikuu cha Dar es salaam. pia ameongeza kusema serikali yake itatoa hela kwa ajiri ya ujenzi wa Hosteli za Wanachuo katika maeneo ya karibu na Chuo na kuwaomba mashirika ya hifadhi ya jamii kujitokeza kuwekeza katika ujenzi wa hosteli hizo


Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)