MASTAA WA UJERUMANI WASHINDWA KUTAMBA MBELE YA POLAND

Ujerumani na Poland wamecheza kwa mara ya kwanza mchezo uliomalizika kwa sare ya bila kufungana baada ya mchezo wao wa Euro 2016 kumalizika huku kila timu ikiwa imeshindwa kupata bao katika kupambana kufuzu hatua ya mtoano utoka kwenye makundi.

Timu zote sasa zinapointi 4 huku zikiwa zimesaliwa na mechi moja mkononi ambao unawezeza kuwahakikishia kufuzu kwa hatua inayofuata huku Switzerland iliyo nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu ikitegemea matokeo mengine hata kama itashinda mchezo wake wa mwisho.

Striker wa Poland Arkadiusz Milik alipoteza nafasi nafasi ya wazi kuifungia timu yake sekunde chache baada ya kuanza kipindi cha pili, mpira wa kichwa alioupiga akiwa hatua nne kutoka golini ukienda nje ya goli wakati kila mtu akiamini nyota huyo angepachika bao.

Wachezaji wawili wa Ujerumani Mario Gotze na Mesut Ozil walishindwa kufunga magoli baada ya Lukasz Fabianski kuchukua nafasi ya Wojciech Szczesny aliyeumia huku mashambuliaji wa Poland Milik akipoteza nafasi nyingine ya wazi kwenye usiku ambao angeiandikia historia nchi yake kwenye uwanja wa Stade de France.

Matokeo hayo yanaisukumiza Ukraine nje ya mashindano hayo kwasababu bado haina pointi hadi sasa.
Habari Kuu Bofya hapa
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top