Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT-Wazalendo Mh: Zitto Kabwe ametoa maoni yake kupitia ukurasa wake wa facebook juu ya mapendekezo ya kutoza kodi kiinua mgongo cha wabunge na posho zingine
Mapendekezo ya kutoza kodi kwenye gratuity ( kiinua mdomo ) kwa Wabunge ni sahihi kwani ni pato ambalo lazima litozwe kodi. Hata hivyo kiini ni kanuni ya kukokotoa kiwango kinacholipwa. Mabadiliko ya maana ni kufuata Sheria kwenye kulipa na kutoza kodi. Vile vile pato hili halipo mwaka ujao wa fedha na halitakuwepo mpaka mwaka 2020. Kwanini lisemwe sasa ni jambo la kushangaza kidogo.
Nadhani pato linalopaswa kutozwa kodi ni Posho ya Vikao ( sitting allowances ). Hili ni pato Kama pato lingine lolote na halilipiwi kodi. Sitting allowance kwa watu wote wanaopata ikitozwa kodi ( kwa sababu inaonyesha haiwezi kufutwa ) itarudisha fedha nyingi Serikalini.