MAJIBU YA PUMA BAADA YA SHUTUMA NYINGI KWA JEZI ZAO ‘FEKI’



Mapema leo nyota wa Uswizi XHERDAN SHAQIRI alikaririwa akisema “Puma hawawezi kutengeneza kondom” baada ya mchezo wao dhidi ya Ufaransa kufuatia kushuhudia jezi za wachezaji wenzake
wanne zikichanika..

Puma ambao makao makuu yao yako nchini Ujerumani, walipata kashafa hiyo baada ya jezi za wachezaji wa Uswizi Breel Embolo, Granit Xhaka, Admir Mehmedi na Blerim Dzemaili kuchanika katika mchezo wa jana dhidi ya Ufaransa uliomalizika kwa suluhu.

Mchezaji wa zamani wa Gary Lineker pia kwenye Twitter yake aliikashfu Puma kwa kusema: “Jezi za timu ya Uswizi zinachanika kama karatasi. Mipira ya Adidas inapasuka. Huwezi kuwekea dhamana bidhaa za Kijerumani!”

Baada ya kashfa hiyo kubwa…..kupitia msemaji wao Kerstin Neuber , Puma wameamua kujitokeza hadharani na kusema: “Timu nyingine tano ambazo zinatumia jezi zetu zimecheza mechi zilizopita bila ya suala hili kutokea.

“Waataamu wetu wa masuala haya wapo makini kufanyia uchunguzi material ya jezi hii. Tutakapolitambua tatizo tutatoa taarifa rasmi.”

Jarida la Blick linadai kwamba kuchanika huko kwa jezi kunatokana na kuzidi kwa joto kwenye matengenezo ya jezi hizo hasa kwenye sehemu ya namba na majina.

Moja ya wachuuzi wa jezi za Puma nchini Uswizi Ramon Serrano amesema: “Ilionekana dhahiri kwamba sehemu ya namba katika jezi ilikuwa imejichora sana kiasi ya kuwa hatarini kuchanika.

“Hasa ukiangalia kwa upande wa Xhaka na Embolo, ilikuwa ni ushahidi tosha kabisa. Kwa kuprint kwenye zaidi ya nyuzi joto 150, lazima kutakuwa na ‘chemical reaction’. Kwa kuongezea tu ni kwamba, ukiangalia jezi zenyewe zinabana sana. Tisheti hazivutiki na kutanuka vizuri kama hapo awali.”
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top