Lowassa awaasa wahitimu wa vyuo vikuu ambao ni wafuasi wa Chadema mikoa ya Dar es salaam na Pwani katika Mahafali yaliofanyika leo


Aliyekuwa Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe.Edward Lowasa leo alikuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu Dar es salaam.
Katika hotuba yake kwa
wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ambao ni wanachama wa CHADEMA ,Mhe.Lowasa amesema ana kila ushahidi kuwa alishinda Uchaguzi Mkuu katika kiti cha urais mwaka jana lakini ameamua kuwa kimya juu ya hilo kwa mustakabali wanchi.

Pia Mh. Lowassa ameikosoa Ripoti ya Jumuiya ya Ulaya kuhusiana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kuwa ilikuwa na dosari nyingi na imetengenezwa katika mazingira ya kukifurahisha chama tawala.
Mhe.Lowasa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani amesema Ripoti hiyo ya Jumuiya ya ulaya ilitakiwa iende mbele zaidi na kuelezea kile kilichofanyika nchini kama kilikuwa ni huru na haki kwa mustakabali wa Demokrasia nchini ambapo pia ameikosoa vikali Tume ya Uchaguzi.

Baadhi ya wanafunzi hao wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu wamemweleza kuwa walikabiliana na wakati mgumu kipindi cha masomo yao hasa baada ya kuweka wazi hisia zao za kuunga mkono upinzani.

HABARI KUU LEO BOFYA HAPA


Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top