KOCHA DUNGA TIMU YA TAIFA BRAZIL ATIMULIWA . HUYU HAPA ANAYEWEZA KUMRITHI

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/05/dunga.jpg
Brazil imemtimua kocha wake Carlos Dunga siku ya leo Jumanne baada ya Selecao kushindwa kufnya vyema na kutupwa nje katika hatua ya makundi katika Copa
America Centenario.
Peru iliwaondoa Brazil kwa kuwafunga 1-0 shukrani pekee kwa goli lilokuwa limejaa utata siku ya Jumapili ambapo ilionekana kugonga mkono wa mshambuliaji Raul Ruidiaz na kuzama kwenye nyavu.

Lakini kwa namna ambayo wamekuwa wakishindwa kupata matokeo ya kuridhisha ikiwa ni pamoja na hii ya kushindwa ilionyesha dhahiri kuwa matokeo ya Brazil yalikuwa hayatoshi kumhakikishia ajira yake Dunga, hivyo Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) likamwondoa kwenye majukumu yake baada ya kurudi kutoka Marekani siku ya Jumanne.

Vyanzo vya karibu na klabu ya Brazil ya Corinthians vimepenyeza habari kuwa CBF tayari imeanza mazungumzo na meneja na kocha wao Tite kuchukua nafasi ya Dunga. Tite pia anaweza kuchukua majukumu ya kuinoa timu ya Olimpiki kuanzia Agosti, wakati wenyeji Brazil watakuwa wakijaribu kutafuta medali ya kwanza ya dhahabu.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Gilmar Rinaldi naye katupiwa virago baada yeye na Dunga kukutana na Rais wa CBF Marco Polo Del Nero Jumanne.

Kauli ya CBF ilisema: “CBF ilitangaza Jumanne kuwa iliamua kuvunja mkataba na watendaji wa benchi la ufundi la timu ya taifa nchini Brazil akiwemo mratibu, Gilmar Rinaldi, kocha Dunga na wafanyakazi wake wote watatakiwa kuachia nafasi zao.

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top