
Ujumbe uliondikwa na Ulimwengu kupitia akaunti yake ya Insta unasomeka hivi: “Mi namwita kiraka@abo Master…sijawahi kumwona akicheza golikipa tu ila sehemu zote anakava… tuko pamoja mwanagu#hainakufeli#hainakufeli ….”
Kabla ya Ulimwengu, Juma Abdul pia ali-post kupitia akaunti yake ya Instagram na kutoa ya moyoni baada ya rafikiyake kutopewa mkataba mwingine wa kuitumikia Yanga mara baada ya ule wa awali kumalizika.
Telela hayupo kwenye kikosi kilichosafiri kwenda Uturuki kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya mchezo wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya MO Bejaia, lakini uongozi wa Yanga haujatoa taarifa rasmi ya kuachana na kiungo huyo aliyedumu kwenye klabu hiyo kwa misimu sita mfululizo.