Euro 2016 zinaanza Leo ambapo wenyeji Ufaransa watapepetana na Romania.Timu zinazoshiriki ni 24 kwa siku 30 katika viwanja 10 vya Ufaransa.
Nyota wanaotegemewa kuonekana ni Nyota wa Real Madrid, ambaye alikuwa kwenye nafasi ya pili ya mchezaji bora wa dunia katika Tuzo za Ballon d'Or, ambaye katika mechi ya kuelekea Euro Ureno wamewapiga bao 7 Estonia naye akatupia mbili Cristiano Ronaldo, anarajiwa kutamba na kikosi chake cha Ureno huku Gareth Bale mchezaji ghali kuliko wote duniani naye akitegemewa kung’ara nan chi yake ya Wales.
Washindi wa Kombe la Dunia Ujerumani wao watakuja na majina kadhaa, Mlinda Mlango wa Bayern Munich Manuel Neuer, Mshambuliaji Thomas Muller na Kiungo wa Real Madrid Toni Kroos. Wafaransa watang’arishwa na kiungo wa Juventus Paul Pogba ambaye kwa sasa anaangaliwa na vilabu vingi vya Ligi Kuu.
Ubelgiji hawako nyuma, watakuwa na Eden Hazard na Kevin de Bruyne wakati Sweden ikimtanguliza nyota wao Zlatan Ibrahimovic.