WATU WENYE ULEMAVU WAJENGEWE MIUNDOMBINU RAFIKI KUPUNGUZA CHANGAMOTO ZA KIMAISHA


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akizungumza watu wenye ulemavu na<Endelea bofya kichwa cha habari hii juu>



Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akifatilia uwasilishwaji wa kanzidata ya watu wenyes ulemavu nchini iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu. 



Bwana Joachim Marege ni mtu mwenye ulemavu asiyeweza kutembea. Baba huyu anakofanyia kazi inabidi apande lifti hadi ghorofa ya kumi. Siku moja nikiwa nimeongozana naye kwenye lifti mara ghafla umeme ukakatika. Baada ya lift kufunguliwa nikamsaidia kutoka kwenye lift na kuendelea na safari yangu lakini kwa ndugu huyu haikuwezekana kuendelea na safari yake kwa kupanda ngazi ilibidi asubiri kwa muda hadi umeme utakaporudi ndo akapanda lift na kwenda ofisini kwake. Hii ni changamoto sana kwa watu wenye ulemavu katika kupata miundombinu rafiki ya kuwawezesha katika shughuli zao za kila siku na ambao idadi yao inaongezeka kila kukicha.

Mnamo Aprili 11 2016 Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakishirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu walizindua kanzi data maalum kwa ajili ya kupata takwimu za watu wenye ulemavu nchini.

Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani, zaidi ya watu bilioni moja dunia sawa na asilimia 15 ya watu wote duniani wanakadiriwa kuwa na aina fulani ya ulemavu. Idadi ya watu wenye ulemavu inaongezeka kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo ajali, majanga ya asili na ya kusababishwa na binadamu, ongezeko la watu hasa wenye umri mkubwa, magonjwa ya kuambukiza, magonjwa ya akili na matatizo sugu ya kiafya.

Kuongezeka huku kwa idadi ya watu wenye ulemavu, kunasababisha mahitaji makubwa ya huduma muhimu za kijamii. Aidha, maisha ya watu wenye ulemavu yanakuwa magumu zaidi kutokana na unanyanyapaa kutoka kwa jamii kwa ujumla, hali ambayo inahitaji mabadiliko ya kimtazamo. Ni ukweli ulio wazi kwamba watu wenye ulemavu hasa katika nchi zinazoendelea kama Tanzania wana matatizo ya upatikanaji wa huduma za kijamii kama vile elimu na afya ikilinganishwa na watu ambao hawana ulemavu.

Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), karibu asilimia 80 ya watu wenye ulemavu wanaishi katika nchi zinazoendelea. Umaskini hupunguza uwezekano wa watu wenye ulemavu kupata huduma za kijamii na haki nyingine za kimsingi. Kwa bahati mbaya programu nyingi za maendeleo zimeshindwa kuzingatia mahitaji maalum ya watu wenye ulemavu kinyume na makubaliano ya kimataifa yanayosisitiza uzingatiaji huo kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Tumeshuhudia majengo yaliyojengwa muda mrefu hata yanayojengwa sasa mengi hayazingatii mahitaji maalum kwa watu wenye ulemavu. Inabidi katika ujenzi miundombinu rafiki kwa wenye ulemevu iwekwe ili kuwapunguzia adha katika maisha watu wenye ulemavu.

Pamoja na umuhimu na uelewa uliopo bado upatikanaji wa takwimu sahihi ni tatizo hasa katika nchi zinazoendelea kama Tanzania. Kwenye ngazi ya kimataifa, bado kuna tofauti kuhusu nini hasa maana ya ulemavu, suala ambalo husababisha ulinganifu wa takwimu kuwa mgumu. Katika ngazi ya kitaifa, taarifa za watu wenye ulemavu hazitoshelezi mahitaji ya kuweka misingi madhubuti ya kupanga na kutekeleza programu za maendeleo zinazolenga kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu.
Credit: Raymond Mushumbusi 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top