LGBT
Kundi moja la nchi 51 za kiislamu limeyazuia mashirika ya kupigania haki za wapenzi wa jinsia moja kushiriki katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi mwezi ujao.
Misri,inayowakilisha mashirika ya <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>Kiislamu ilimuandikia rais wa mkutano huo wakitaka makundi hayo kuzuiwa kushiriki.
Marekani,Muungano wa Ulaya na maafisa wa Canada wamemuamdikia rais wa shirika hilo lenye wanachama 193 wakipinga kushiriki kwa watu hao.
Wawakilishi wa Misri hawakutoa sababu wa kutaka makundi hayo kupigwa marufuku.Mkutano wa UN
Balozi wa Marekani Samantha Power amesema kuwa makundi hayo yalionekana kuchaguliwa kwa kushiriki kwao katika harakati za wapenzi wa jinsia moja na watu wanaobadili jinsia.
''Huku ikiwa watu wanaobadili jinsia wana uwezekano mara 49 wa kuishi na virusi vya ukimwi ikilinganishwa na idadi ya watu wa kawaida,kuzuiliwa kwao katika mkutano mkubwa kama huo kutaathiri maendeleo katika vita dhidi ya ugonjwa huo'',alisema Bi Power katika barua aliyomwandikia rais wa mkutano huo Mogenns Lykketoft.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)