Wakazi wa DSM wahimizwa kuunga mkono na kuchangia Madawati

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameendelea kuwahamasisha wakazi wa Dar es salaam, wadau wa Maendeleo yakiwemo mashirika na taasisi kuunga mkono harakati za kuondoa tatizo la upungufu wa madawati, linalozikabili shule mbalimbali za <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>msingi na sekondari mkoani Dar es Salaam.

Akizungumzia kampeni ya uchangiaji madawati iliyoandaliwa na kituo hiki cha Channel ten kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es slaam, Bw. Makonda amesema pamoja na juhudi zinazoendelea, hadi sasa bado kuna mahitaji ya madawati elfu 66 kwa shule za msingi na upande za sekondari madawati elfu 34 pamoja na mahitaji ya vyumba vya madarasa.

Awali akitoa taarifa ya maandalizi ya harambee iliyopangwa kufanyika mwezi ujao, Mwenyekiti wa kamati ya kampeni hiyo Hamid Abdulrahman alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa mwitikio ni mkubwa baada ya wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara kuunga mkono kampeni hiyo inayolenga kupata jumla ya madawati laki moja.

Kwa yeyote atakaeguswa na kampeni hiyo anaombwa kuchangia kupitia akaunti namba HARAMBEE MADAWATI TANZANIA TRUST TAWI LA NMB OHIO akaunti namba 24110000404 Dar es salaam.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top