Usalama wa wasiwasi kwa wananchi wanaotumia barabara za mwendo kasi.


Hali ya Usalama kwa wananchi wa jiji la Dar es salaam wanaotumia barabara za mwendo kasi wakati wa kuvuka imeonekana kuwa ya <endelee bofya kichwa cha habari hii juu>wasiwasi baada ya wananachi hao kutumia barabara hizo kuvuka kwa miguu badala ya kutumia madaraja maalum ya kuvukia yaliyowekwa katika vituo mbalimbali vya mabasi hayo.

Licha ya Mamlaka husika inayoshughulikia Mabasi hayo kuweka utaratibu maalum wa kuvuka na kuwataka wananachi kutotumia barabara hizo kuvuka kutoka upande mmoja kwenda mwingine, utaratibu ambao umekuwa mgumu kufuatwa..

Channel ten ilifika katika kituo cha mabasi ya mwendo kasi kilichopo kimara jijini Dar es salaam na kushuhudia watu mbalimbali wakivuka kupitia barabara ya mwendo kasi huku wachache wakitumia daraja lililowekwa na UDARAT ambapo katika mahojiano na Channel ten wananachi hao wamedai kuwa licha ya kufahamu kuwa utumiaji wa barabara hizo kunahatarisha usalama wao lakini wanavuka barabara hizo ili kurahisisha uvukaji kutokana na madaraja yaliyowekwa kuwa na mzunguko mrefu ambao baadhi ya watu wakiwemo walemavu na wazee kushindwa kutumia madaraja hayo.

Hali ya Usafiri wa mabasi ya mwendo kasi imezidi kuimarika tangu kuanza kwa huduma hiyo licha ya changamoto mbalimbali ambazo mamlaka husika tayari zimeahidi kuzishughulikia.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top