Mwenge wa uhuru umeendelea kukimbizwa katika jiji la Dar es salaam ambapo leo umezindua miradi saba ya maendeleo katika manispaa ya Ilala.
Akizungumza wakati wa uzinduzi jengo la <endelee bofya kichwa cha habari hii juu>hospitali ya Regency, kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa George Mbijima amesema serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na sekta bianfsi katika kusaidia maendeleo kwa jamii.
Bwana Mbijima ametoa wito kwa wauguzi nchini kutoa huduma yenye ukarimu kwa wagonjwa pindi wanapofika hospitali kupata huduma za matibabu.
Akisoma risala mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa meneja rasiliamali watu Thabithy Bashiri ameiomba serikali kuipandisha hadhi hospitali ya Regency kutoka hadhi ya mkoa mpaka hadhi ya kitaifa.
Miradi hiyo saba iliyozinduliwa na mwenge wa uhuru ni pamoja na upanuzi wa hospitali ya Regency, ujenzi wa zahanati ya mganga chanika, mradi wa ufugaji wa samaki wa eden Aqua ltd Pugu Kinyamwenzi, ujenzi wa soko la Kigogofresh Pug na ujenzi wa shule ya msingi maghorofani Gongo la Mboto jeshini.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)