Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) Jamal Malinzi
PAZIA LIGI KUU YA VODACOM KUFUNGWA KESHO
Michezo ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kufanyika kesho Jumapili, Mei 22, 2016 kwa timu zote 16 kutinga katika viwanja vinane tofauti kumaliza ngwe ya msimu wa 2015/16.
Michezo itakayopigwa kesho ni <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>pamoja na Simba itakayokipiga na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Azam FC ambayo inawania nafasi ya pili kama Simba, itakipiga na African Sports kwenye Uwanja wa Azam Complex, ulioko Chamazi, Mbagala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Kwa taarifa zaidi fuata link hapo chini
AIRTEL TANZANIA YAPANGA MIKAKATI YA MAENDELEO SOKA LA VIJANA
Kampuni ya Airtel Tanzania jana Ijumaa Mei 20, 2016 imekutana na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) kuzungumzia mipango ya maendeleo wa mpira wa miguu nchini ikiwa ni pamoja na michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars inayotarajiwa kuanza Juni mwaka huu.
Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine ambaye ndio aliongoza kikao hicho, alitoa shukrani ka kampuni ya Airtel kwa kuwekeza kwenye soka la vijana ambalo ndio msingi wa kukuza mpira wa miguu nchini. “Naamini ya kwamba kwa kuendelea kuwekeza kwenye soka la vijana, tutaweza kufika mbali kwa kupata matokeo mazuri.”
Kwa taarifa zaidi fuata link hapo chini
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)