Serikali yamwaga maelfu ya ajira kwa kada ya walimu

Walimu 35,411 nchini wataajiriwa katika shule za msingi na sekondari katika mwaka wa fedha 2016/2017.


Watakaokaidi kwenda kuripoti katika mikoa ya <Endelea bofya kichwa cha habari hii juu>
pembezoni, hawataajiriwa na serikali.


Hatua hiyo imeelezwa kwamba imetokana na serikali kupokea maombi mengi ya kazi kwa walimu, ambao mwaka jana hawakuripoti katika vituo walivyopangiwa pembezoni mwa miji kwa kutegemea kuajiriwa na shule binafsi, lakini hawakufanikiwa.


Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo alisema hayo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF) aliyetaka kufahamu serikali inafanya nini kwa walimu waliopangiwa kwenda mikoa ya pembezoni, ikiwemo Lindi na kwingineko, lakini hawakuripoti.


Jaffo alisema ni kweli kuna walimu wengi ambao hawakuripoti katika mikoa ya pembezoni. Alisema si Lindi peke yake, bali na mikoa mingine, ikiwemo Katavi na Kigoma.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top