Rooney sasa kuwa kiungo timu ya taifa


Wayne Rooney
Wayne Rooney sio tena mshambuliaji namba moja katika timu ya taifa ya Uingereza,amesema nahodha wa <Endelea bofya kichwa cha habari hii juu>


Rooney ambaye anaongoza rekodi ya ufungaji wa muda wote ametajwa katika kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya michuano ya Euro 2016.


Shearer amesema Rooney mwenye miaka 30 anafaa zaidi katika nafasi ya kiungo nyuma ya Harry Kane na Jamie Vardy. ''Lazima pawepo nafasi kwa ajili ya nahodha wa timu na vizuri imekuwepo''alisema.Lakini siku za Wayne kuw mshambuliaji wa kwanza zimeisha. ''Nafikiri Harry Kane na Jamie Vardy wanapaswa kuanza mbele lakini bado Rooney ana nafasi kubwa ya kucheza ama namba kumi ama kiungo wa kati. Rooney ni miongoni mwa washambuliaji watano walioitwa katika kikosi cha Roy Hodson siku ya jumatatu kwa ajili ya michuano ya Euro 2016.Wengine ni Harry Kane,Jamie Vardy, Daniel Sturridge na Marcus Rashford.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top