Mji wa India wavunja rekodi ya vipimo vya joto

Image copyrightEPAImage captionJoto kali India

Mji mmoja katika jimbo la Rajasthan nchini India umevunja rekodi baada ya kusajili vipimo vya juu vya<endelea bofya kichwa cha habari hii juu> joto vya hadi 51 C,ikiwa ni vya juu tangu kuanzishwa kwa rekodi za viwango hivyo ,kulingana na ofisi ya hali ya hewa.

Rekodi hiyo mpya katika eneo la Phalodi katika jimbo hilo la jangwa inajiri wakati ambapo kuna wimbi la mvuke joto kali nchini India.

Rekodi ya awali ya vipimo vya juu vya joto ilikuwa 50.6C mnamo mwaka 1956.

Wimbi hilo la Joto hilo limekumba eneo kubwa la India Kaskazini ambapo joto limepita vipimo vya 40C kwa wiki kadhaa sasa.

Wakati wa msimu wa upepo nchini India huwa na jua kali na kupanda kwa vipimo vya joto ,lakini viwango vya joto vinavyopanda hadi 50C sio vya kawaida.

Murari Lal Thanvi,shahidi mmoja huko Phalodi amiambia BBC ,kwamba alijaribu kukaa nje siku ya Ijumaa.Joto kali India

''Hata simu yangu ilisalimu amri na kuwacha kufanya kazi nilipokuwa nikipiga picha'',alisema.

Nilifanikiwa kuiwasha simu yangu baada ya kuiweka kitambaa chenye maji kwa takriban dakika 20-25.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top