Tai akiwa anapaa
Kuku na vifaranga vyake
Siku moja nilisoma habari iliyosisisimua moyo wangu na kunifanya nifanye maamuzi mapya kuhusiana na aina ya
maisha ninayotaka kuyaishi kuanzia siku hiyo.Kulikuwa na mfugaji mmoja ambaye alikuwa anafuga kuku wengi kijijini,siku moja kwa bahati mbaya aliokota yai la tai akiwa njiani kutoka shambani.Akaamua kulichukua yai lile na akaliweka kwa kuku mmoja wapo ambaye alikuwa anaatamia mayai yake.
Baada ya muda kupita,kuku yule aliyatotoa mayai yale likiwemo na lile yai la tai.Hivyo tai akazaliwa pamoja na vifaranga wengine bila kujua kuwa yeye ni tai.Miaka mingi ikapita bila yule mtoto tai kutambua kuwa ana uwezo wa kuruka juu sana na ana nguvu ya kula vyakula “fresh” na sio kukimbilia katika mashimo ya taka kama wanavyofanya kuku wengine.
Siku moja akiwa anaendelea kutafuta chakula kwa kuparua chini TAI mkubwa akapita akiwa anaruka kwa madaa.Mtoto wa tai akawaambia vifaranga wenzake,natamani siku moja niweze kuruka kama yule pale-Wenzake wakamwambia hilo haliwezekani na kuanza kumcheka na kumwambia aache kunia makuu.Hadi mtoto tai anazeeka na akafa hakuwai kuruka ingawa alikuwa ana uwezo wa kuruka.
Ndivyo ilivyo katika maisha yetu.Kila mmoja wetu amezaliwa na uwezo mkubwa na wa kipekee uliojificha ndani yake lakini kwa sababu ya aina ya watu wanaotuzunguka huwa tunajikuta tunaishia kuwa watu wa kawaida,kuweka malengo ya kawaida na kuwa na ndoto ndogondogo kama za kuku.Mara nyingi malengo yetu yamejikita kwa kujilinganisha na watu wanaotuzunguka(niwe na nyumba,niwe na gari,watoto waende shule nzuri basi)-Hii hutokana na aina ya masiha ya Marafiki zetu,jamaa zetu na wazazi wetu,na kwa kufanya hivyo tunajikuta tunaishia kuishi maisha ya kinyonge kama alivyoishi tai mtoto.
Tai mtoto alitamani kuweza kuruka juu kama alivyokuwa ameona TAI wakubwa wakiwa wanaruka lakini hakuwahi kujaribu kufanya hivyo.Mara nyingi huwa tunatamani kufanikiwa katika mambo fulani au kufikia malengo fulani makubwa katika maisha yetu lakini tatizo kubwa ni kuwa huwa hatujaribu hata kuchukua hatua ya kwanza.Hebu fikriria kama tai mtoto angejaribu kuruka ghafla angejikuta amesharuka juu na asingekufa akiishi kama kuku.Usiendelee kutamani kuwa kama TAI,chukua hatua za kuruka kama tai na ujaribu kufanya utashangaa, uwezo unaoutamani uko ndani yako tayari.
Kila wakati Tai mtoto alipojaribu kuruka,kuku wanaomzunguka walimkatisha tamaa.Kila wakati utakapojaribu kuwa na malengo na ndoto kubwa Zaidi ya wanaokuzunguka utakatishwa tamaa na wao.Kila utakaposema nitakuwa mtu mkubwa maishani,nitamiliki biashara kubwa ama nitakuwa tajiri sana-Kuku huwa wana tabia ya kukukatisha tamaa kwamba”sahau,hilo haliwezekani”.
Usikubali kuishi maisha yako kwa kuwaridhisha kuku wanaokuzunguka,usikubali kufa ukiwa kuku wakati wewe uliumbwa kuwa tai,usikubali kukatishwa tamaa na maneno ya kuku wakati wewe sio mmoja wao.Leo angalia kushoto na kulia kwako,angalia ndoto yako na tazama malengo yako na ujiambie”Nimeumbwa akuwa Tai,sitakubali Kuishi kama Kuku”.
Leo amua kuiaga familia ya Kuku na anza maisha mapya kama tai.
Imo nguvu ndani yako,umo uwezo ndani yako,vimo vipaji ndani yako ambavyo ukiamua kuvitumia bila uoga ama kukatishwa tamaa utashangaa jinsi utakavyopaa juu na kuwaacha kuku wakikushangaa.Mwaka huu,usikubali kuishi kama kuku.
Kila unapokuatana na mtu anayekuambia huwezi,haiwezekani,hautafanikiwa,hilo ni gumu-Ujue kuwa huyo ni kuku anajaribu kukufanya uwe mmoja wao-USIKUBALI.
Kuanzia leo amua kuishi kama TAI na kila KUKU unayekutana usikubali akukatishe TAMAA.Akianza kukukatisha tamaa mwambie-KUKU ndio HAWAWEZI ila TAI huwa TUNAWEZA.
Kumbuka kuwa Ndoto Yako Inawezekana.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)