Mkutano wa wakuu wa Majeshi ya nchi kavu Afrika kujadili changamoto zinazoyakabili majeshi hayo unamalizika leo, Arusha Tanzania.
Kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi, Luteni Kanali Ngeleba Lubinga, viongozi hao wamepeana uzoefu wa kukabiliana na ugaidi, mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu, ikiwemo usafirishaji watoto pamoja na dawa za kulevya.
Mkutano huo, ulioanza Mei 16 na Kufunguliwana Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi nchini Tanzania, umewashirikisha wakuu wa majeshi ya nchi kavu zaidi ya 38.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)