MADEREVA wa magari waaswa kuwa makini wakati wakiendesha magari hasa katika makutano ya<endelea bofya kichwa cha habari hii juu> magari ya mwendo wa haraka yanayotoa huduma za usafari jijini Dares Salaam.
Hayo yamesikika na shuhuda mmoja wakati wa ajali iliyotokea katika makutano ya Barabara ya BRT na Bibititi Mohamed eneo la chuo cha CBE jijini Dar es Salaam leo.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 5 katika eneo la Chuo cha CBE jijini Dar es Salaam leo kati ya Gari lenye namba za usajili T 713 DFC na gari la mwendo wa haraka lililokuwa likitokea Kivukoni.
Ajali imetokea katika makutano ya barabara ya Bibititi Mohamed na barabara ya BRT maeneo ya chuo cha CBE jijini Dar es Salaam ikiwa ajari hiyo imetokea kati ya Gari lenye namba za usajili T 713 DFC lililokuwa likitokea Mnazi mmoja kuelekea Maktaba na kugonga gari la mwendo wa haraka lililokuwa likitokea Kivukoni.
Chanzo cha ajali hiyo ni Mataa ya makutano ya barabara hiyo kutokufanya kazi ya kuongoza magari.
Gari lenye namba za usajili T 713 DFC likiwa limeharibika mara baada ya kugonga gari la Mwendo wa haraka katika eneo la chuo cha CBE jijini Dar es Salaam leo.
Gari lenye namba za usajili T 713 DFC ambalo limeharibika kwa kugonga gari la mwendo wa haraka likivutwa na Breakdown kuondolewa eneo palipokuwa na ajali hiyo eneo chuo cha CBE na katika makutano ya barabara ya BRT na Bibititi Mohamed jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)