Wanamgambo wanasema wako kwenye kampeni ya kutaka wenyeji wa Niger Delta kupata mgao wa utajiri wa mafuta.
Kiwanda cha mafuta cha<endelea bofya kichwa cha habari hii juu> kampuni ya Chevron nchini Nigeria kimeshambuliwa na wanamgambo.
Kampuni hiyo ya Marekani inaripotiwa kufuta shughulia zake kufuatia uvamizi huo.
Kundi linalojiita Niger Delta Avengers, lililisema kuwa lililipua kituo cha umeme huku wenyeji wakisema kuwa walisikia mlipuko.Mafuta yanachangia asilimia sabini ya pato la taifa nchini Nigeria.
Avengers wanasema kuwa wako kwenye kampeni ya kutaka wenyeji wa Niger Delta kupata mgao wa utajiri wa mafuta.
Mauzo ya mafuta yasiyosafishwa yanachangia asilimia sabini ya pato la taifa nchini Nigeria, nchi yenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)