IDD AZZAN AKUBALI YAISHE, AINYOFOA KESI YAKE YA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI

ALIYEKUWA Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan ameinyofoa kesi yake ya uchaguzi mahakamani aliyokuwa ameifungua ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Mbunge wa <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>
Chama cha Wananchi (CUF), Maulid Mtulia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. 

Azzan amesema kuwa kuondoa kwa kesi hiyo ni kutaka kujipa muda wa kufanya shughuli zake na Mbunge wa Kinondoni aendelee kuhudumia wananchi wa Kinondoni kutokana na watu nia ni kuwatumikia wananchi. 

Uamuzi huo umetolewa leo na Azzan kupitia mwanasheria wake mbele Jaji wa Mahakama Kuu ya Mbeya, Jaji Chochi ambapo mahakama ilikubali maamuzi hayo yaliyolewa na upande wa mashitaka. 

Naye Wakili wa Mbunge wa Kinondoni, Juma Nassoro amesema kuwa walikuwa wamejipanga kuhakikisha kesi hiyo wanashinda lakini kutokana na Azzan kuomba kuiondoa kesi hiyo,basi Mbunge Mtulia aendelee kuwahudumia wananchi. 

Nae Mbunge wa Jimbo hilo, Mtulia amesema kuwa ametumia muda mwingi kuja kusikiliza kesi na kushindwa kuchangia katika bunge la bajeti linaloendelea baadhi ya wizara. 

Amesema sasa atahudumia wananchi wake vizuri kutokana na muda atautumia ofisini ikiwa ni pamoja na ushiriki katika bunge kuwakilisha wanakindoni katika matatizo yanayo wakabili.
Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan akimpongeza Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia kufuatia kuiondoa kesi yake ya uchaguzi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na mbunge huyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia akiingia mahakamani katika kesi ya uchaguzi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Idd Azzan leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan akiingia mahakamani, ambapo alifungua kesi ya uchaguzi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa CUF, Maulidi Mtulia leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watu waliofika kuisikiliza kesi hiyo

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top