Hii ndiyo sababu ya Hotuba ya Godbless Lema kuzuiwa kusomwa asubuhi

Hotuba ya Godbless Lema, Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya <Endelea bofya kichwa cha habari hii juu> 
Nchi ilizuiliwa leo asubuhi kusomwa Bungeni hadi ipitiwe upya na kamati ya kanuni.


Bunge liliahirishwa leo asubuhi hadi saa 10 jioni baada ya kuzuia kusomwa kwa hotuba hiyo kwa madai kwamba, ina maneno yanayohitajika kuondolewa ili ikidhi matakwa baada ya kupitiwa na Kamati ya Kanuni.


Ndani ya Hotuba ya Lema kipo kipengelea kinachoelezea sakata la makataba tata wa Kampuni ya Lugumi ambapo Kamati ya Mambo ya Ndani ilielezwa suala hilo kutojadiliwa bungeni kwa madai tayari lilikuwa limeanza kuchunguzwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).


Kipengele kinachohusu mkataba wa Kampuni ya Lugumu kipo kwenye sehemu ya tano inayoeleza Mikataba Tata ya Jeshi la Polisi.


Kwa muda mrefu mkataba huo uliotolewa na Jeshi la Polisi nchini kwa Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd wenye thamani ya Sh 37 bilioni umedaiwa kuwa na harufu ya ufisadi.


Mwaka 2011, kampuni hiyo ilipewa zabuni ya kufunga mashine za alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchini na kulipwa Sh 34 bilioni kati ya Sh 37 bilioni sawa na asilimia 99 ya malipo yote.


Mambo mengine yaliyosababisha hotuba hiyo izuiliwe ni Uuzwaji wa nyumba uliomtaja Rais John Magufuli moja kwa moja, Rushwa na bunge kutumika kuwalinda watuhumiwa , tabia ya Rais na usalama wa nchi na mwisho ni kuwataja viongozi wa juu wa serikali kwa maneno ya dhihaka.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top